Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amemzawadia Askari Polisi PC Alphonce Daniel
Mwambenga sh. 200,000 kutokana na ujasiri wake wa kumdhibiti kwa
kumkanyaga nyoka mkubwa aliyekuwa akieleakea jukwaa kuu wakati Waziri
Mkuu akihutubia katika Kilele cha Wiki ya Viziwi Duniani kwenye Uwanja
wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa, Sepotemba 28, 2019. Kitendo hicho
kilifanyika kimyakimya hivyo hapakuwa na taharuki yoyote . Pichani,
Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi Mwambenga fedha hizo. Wapili kulia ni
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu, Stella Ikupa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara y a
Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dkt.Avemaria Semakafu. Wa tatu kushoto
ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamkahanga.
Askari Mwambenga akiwa amemkanyaga nyoka huyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Nyoka akiuawa na baada ya kuuawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Sheria inasemaje katika kulomda wanyama pori?
ReplyDeleteIlipaswa nyoka huyo akamatwe kiutaalamu na kurudishwa kwenye mapori.