Madarasa Manne (4) yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Kibindu kwa Msaada wa TANAPA yamekamilika na yameanza kutumika katika Jimbo la Chalinze,Mkoani Pwani |
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete akizungumza na wananchi (hawapo kwenye picha) katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika jimbo hilo,Mkoani Pwani |
Muonekano wa kituo cha afya Kibindu ambapo Serikali ilitoa fedha shilingi milioni 400 kufanikisha ujenzi huo katika Jimbo la Chalinze mkoani Pwani. |
Naibu Katibu Mkuu Tamisemi-Afya Dr. Dorothy Gwajima na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete wakikagua ramani katika Hosptali ya Wilaya ya Chalinze alipofanya ziara Mkoani Pwani |
Kwa
upande wa vituo vya Afya amesema kazi inaendelea kwa kila Kata ambapo
amesema mpaka sasa bado kata tatu ambazo ujenzi wake uko mbioni kuanza na kuongeza kuwa Serikali imetenga 1.5 Billion kwa ajili ya Upanuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze.
Aidha amesema kwa upande wa elimu kumejengwa vyumba vya madarasa 48,na kwa upande wa umeme umesambazwa katika eneo kubwa katika jimbo la Chalinze.
Ridhiwani
amesema kuwa Serikali imepanga kutumia shilingi 158.5 Milioni kwa ajili
ya ujenzi wa barabara za mji wa Chalinze ambazo zitajengwa kwa kiwango
cha lami na ujenzi wa madaraja madogo.
Muonekano wa kituo cha afya Kibindu ambapo Serikali ilitoa fedha shilingi milioni 400 kufanikisha ujenzi huo katika Jimbo la Chalinze mkoani Pwani. |
Mbunge wa Jimbo wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akikagua kituo cha afya Kibindu ambapo Serikali ilitoa fedha shilingi milioni 400 kufanikisha ujenzi huo. |
Mbunge huyo ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuipatia Chalinze Shilingi Bilioni 16 kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji ambapo fedha hizo zinakwenda kumaliza tatizo la maji Chalinze na maeneo ya jirani ikiwemo Ngerengere na Magindu kwa upande wa Kibaha Vijijini.
Mbunge huyo pia amewapongeza wanawake kwa jinsi wananvyokuwa mstari wa mbele katika ufanisi wao wa kuchangamkia fursa ndondogo za halmashauri.
Amesema hadi sasa vikundi zaidi ya 80 vya wanawake vimeweza kufikiwa katima kata mbalimbali na kupongeza namna wakinamama hao wanavyorudisha mikopo ili watu wengine weweze kukupo kufanya shughuli za maendeleo na kujipatia kipato.
No comments:
Post a Comment