Waziri
wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akizungumza na Waandishi wa
Habari juu ya kongamano la biashara baina ya Tanzania na Uganda.
Mratibu
wa Kongamano la biashara baina ya Tanzania na Uganda Ali Gugu
akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema Jijini Dar es salaam
Na Mwandishiwetu
WAZIRI
wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewataka wafanyabiashara wa
Tanzania kujitokeza Kwa wingi kushiriki katika kongamano la biashara la
Tanzania na Uganda linalotaraji kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu
Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Mapema leo Jijini hapa Bashungwa amesema
kongamano hilo ambalo litafunguliwa na kuhudhuliwa na wakuu
wa nchi zote Mbili Tanzania na Uganda.
"Rais
Magufuli amemualika Rais Museveni wa Uganda katika ufunguzi wa mkutano
hii ambao utawashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 1000 ambao watapata
nafasi ya kujadili namna ya kuongeza biashara mpya baina ya nchi hizi
Mbili" amesema Waziri Bashungwa.
Aidha
Waziri Bashungwa ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya
ziwa ambao wengi wao ndio wamekuwa wakifanya biashara Moja kwa Moja na
nchi za jirani hili waweze kupata mtandao mpya wa kibiashara.
Ametaja
muungano wa kimtandao baina ya Tanzania na Uganda utafungua njia mpya
ya Biashara hadi Sudan ya kusini ambao wamekuwa wakifanya biashara na
Uganda kila uchwao.
Ametaja
muungano wa kibiashara baina ya nchi hizi Mbili utaongeza mabilioni kwa
nchi yetu ya Tanzania kwani mpaka Sasa sisi ndio tumekuwa tukiuza zaidi
kwao kuliko wao kuuza kwetu.
Amesema
kuwa Uganda imekuwa ikitegemea mazao ya chakula kutoka hivyo wauzaji wa
nafaka na Wasindikaji wa vyakula wanatakiwa kutumia fursa hii vizuri
kwa kutanua masoko yao.
Amemaliza kwa kutoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza Kwa wingi katika kongamano hili.
No comments:
Post a Comment