Waombaji Mikopo Kurekebisha Taarifa
Jumatatu, Septemba 23, 2019
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda
kuwajulisha waombaji wote wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 kuwa
kwa sasa HESLB inaendelea na kazi ya uhakiki (verification of
online-submitted applications) wa maombi yaliyowasilishwa ambayo
itakamilika Jumapili, Septemba 29, 2019.
Baada ya kukamilika kwa kazi ya uhakiki, HESLB itatoa fursa ya siku nne, kuanzia Jumatatu, Septemba 30 hadi Alhamisi, Oktoba 3, 2019 kwa waombaji mikopo ambao maombi yao yatakuwa yamebainika kuwa na upungufu kufanya marekebisho.
Taarifa hii inatolewa kufuatia HESLB kupokea maoni na maswali kupitia
barua pepe na simu kuhusu hatua iliyofikiwa katika uhakiki na uchambuzi
wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu yaliyowasilishwa HESLB.
Waombaji mikopo wote wanashauriwa kutembelea tovuti yetu (www.heslb.go.tz) au kuingia katika akaunti zao waliozoombea mkopo kupitia mfumo wa uombaji mkopo (www.olas.heslb.go.tz) kuanzia Septemba 30, 2019 ili
kupata mwongozo wa kufanya marekebisho kwa njia ya mtandao. Baada ya
kuingia, watapata ujumbe iwapo maombi yao yamekamilika au yanahitaji
marekebisho.
HESLB imejipanga kuhakikisha kazi yote ya uhakiki na uchambuzi wa maombi yote ya mikopo inakamilika ifikapo Oktoba 6, 2019 ili
wanafunzi wahitaji wapangiwe mikopo, wapate taarifa na fedha za mikopo
zitumwe vyuoni kabla ya vyuo kufunguliwa katika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, 2019.
Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya HESLB (www.hesl.go.tz).
Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru,
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wa-nafunzi wa Elimu ya Juu
No comments:
Post a Comment