Watanzania 703 Kutoka mikoa 22 Tanzania tayari
wamejisajili kushiriki kongomano la Biashara Tanzania na Uganda la tarehe 6
- 7 Septemba 2019 katika ukumbi wa kimatafa wa mikutano wa Mwalimu Julius
Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es
Salaam.
Takwimu za Washiriki kutoka katika mtandao wa Kujisajili wa www.businessforum.biz , Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa kuwa na
washiriki 588, ukifuatiwa na Mkoa wa Pwani washiriki 19, Mwanza washiriki 11,
Songwe na Tanga washiriki 8 kila Mkoa Ikifuatiwa na Mkoa wa Arusha na Kagera
wenye washiriki 7 kila mkoa. Mkoa mingine wameomba washiriki chini ya saba.
Kutoka Zanzibar washiriki kutoka mikoa miwili
wameomba kushiriki Kongamano hilo, Mkoa hiyo ni Mjini Magharibi na Unguja
Kaskazini.
Vile vile washiriki 17 kutoka Tanzania
wameomba kutoka bila kutaja mikoa
wanayotoka. Hivyo kufanya jumla wa Watanzani 703 kuwa wamejisajili Kushiriki
Kongamano hilo.
Malengo ya waandaaji wa kongamano hilo ilikuwa
ni kuwa na Washiriki 1000, Hivyo lengo limefikia kwa kusajili washiriki 703
kutoka Tanzania huku Uganda Ikisajili Washiki 300, Hivyo tukio la usajili limefanikiwa
kwa zaidi ya asilimia 100.
Katika kongamano hili kunatarajiwa kutakuwa na
Nchi mbili, Wakuu wa Nchi (marais) wawili, Mawaziri 30, Vikao vya jumla vinne,
Paneli 16, Biashara 250, wataofanya maonyesho 25 na washiriki 1000.
Mkutano wa Biashara wa Tanzania na Uganda unawaweka pamoja
wafanyabiashara kutoka Uganda na Tanzania, wachambuzi wa mambo, wachumi,
wataalamu wa sheria, mashirika ya kimataifa, mashirika ya kitaifa, washirika wa
maendeleo na taasisi za habari.
#UGTZBusinessForum2019 #UGTZBusinessForum #TZUGBusinessForum
#TZUGBusinessForum2019
x
No comments:
Post a Comment