Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas
Ndumbaro akiwasilisha pendekezo la Kiswahili kutumika katika ukanda wa
maziwa makuu mjini Brazzaville jana
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas
Ndumbaro akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Vicente
Muanda wakiwa katika ukumbi wa mikutano, mjini Brazzaville jana
Balozi
wa Tanzania Nchini DRC Luteni. Jen. Paul Mella akimueleza jambo balozi
wa sudan wakati wa mkutano wa ukanda wa maziwa makuu mjini Brazzaville
jana
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu wakifuatilia mkutano ulifanyika jana Brazzaville jana
Mawaziri
wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu wakiwa
katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Bwn. Clement
Mouamba jijini Brazzaville jana
…………………….
Na Mwandishi wetu, Brazzaville,
Katika
jitihada za kukuza lugha ya Kiswahili barani Afrika, Tanzania imeziomba
nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu kuanza kutumia lugha ya
Kiswahili kama lugha rasmi na lugha ya kazi
Wito
huo umetolewa katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi
wanachama wa ukanda wa maziwa makuu, uliofanyika mjini Brazzaville leo
na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.
Damas Ndumbaro
“Tumewaomba
wenzetu wa maziwa makuu wakubali lugha ya Kiswahili kutumika kama lugha
rasmi na lugha ya kazi katika nchi zote za maziwa makuu. Pia nchi sita
ambazo zipo hapa na hazijaridhia mabadiliko ya mkataba wa Afrika
kuruhusu Kiswahili kutumika kama lugha rasmi katika Afrika (AU) nchi
hizo zimetuhakikishia kuwa zitaridhia mabadiliko hayo ili kuhakikisha
kuwa Kiswahili kinaanza kutumika kama lugha rasmi ya kazi,” Alisema Dkt.
Ndumbaro
Kwa
mujibu wa Waziri Ndumbaro, matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ukanda
huo ni fursa ambayo italeta umoja wa kitaifa, na katika ukanda wa maziwa
makuu lakini pia umuhimu wa Kiswahili kwamba ni lugha pekee ambayo
haina uhusiano na ukoloni barani afrika.
“Tunatumaini
kwamba tutazipata sahihi za nchi sita na tukisha zipata tutabakiwa na
sahihi ya nchi moja tu ili Kiswahili kiwe rasmi lugha ya kazi katika
mikutano itakayo kuwa inafanyika barani Afrika,” aliongeza Dkt.
Ndumbaro
Nchi
sita ambazo hazijaridhia mabadiliko ya mkataba wa Afrika kuhakikisha
kuwa Kiswahili kinatumika kama lugha rasmi ya kazi ni pamoja na Angola,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudani, Uganda na Zambia.
Kwa
sasa hivi ni lugha rasmi lakini siyo lugha ya kazi kwa hiyo tumekwenda
vizuri kwenye Kiswahili tunaamini ni fursa nzuri ya kuanza kukuza lugha
ya Kiswahili katika bara la Afrika
Wakati
huo huo, Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa, katika mkutano huo nchi
wanachama waliweza kuongelea agenda kuu za nchi wananchama wa ukanda wa
maziwa makuu ambazo ni Amani, Utulivu na Usalama hususani katika eneo la
mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Sanjari
na hilo, nchi nyingi zimeusifu uongozi wa Rais wa DRC, Felix Tshisekedi
kuwa tangu alipoingia madarakani amejitahidhi kuhakikisha kuwa kuna
kuwa na amnai ndani ya DRC pamoja na majirani zake. Pia Uganda, Rwanda
pamoja na Angola zimesifiwa kufanikisha kusaini makubalianao ya kuleta
amanai kati ya Uganda na Rwanda.
Akiongea
awali wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje Mgeni
rasmi ambae alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Bwn. Clement
Mouamba alisema kuwa mkutano wa leo, umelenga kuisaidia nchi ya DRC
katika changamoto inazopitia hasa katika ukanda wa mashariki.
“Nawapongeza
sana kwa kazi ambayo mmekuwa mkiifanya kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali katika kuhakikisha kuwa ugonjwa wa ebola unatokomezwa, kwani
naamini kuwa umoja wetu tunaweza,” alisema Mouamba.
Aliongeza
kwa kuzitaka nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu kuendelea kulinda
amanai na umoja walionao ili kuweza kuendelea na shughuli mbalimbali za
maendeleo kwani bila amani ni vigumu sana kwa umoja huo kuendelea.
Kwa
upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianao wa Jamhuri ya Kongo,
ambae pia alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo Mhe. Jean Claude Gakosso
aliwasisitiza mawaziri wa nchi wanachama kuwa amani na umoja katika
ukanda huo ni nguzo muhimu sana na hivyo waendelee kuishika amani hiyo.
Pia
aligusia ugonjwa wa ebola na kuwataka nchi wanachama kutokata tama ya
kupambana na ugonjwa huo licha ya changamoto zinazojitokeza.
“Juhudi
mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya DRC hadi sasa kwa
kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na wadau wengine
katika kupambana na ugonjwa huo ni kutoa chanjo ya kinga ya ugonjwa huo
na elimu kwa wananchi wa maeneo yaliyoathirika na ugionjwa huo” alisema
Waziri Gakosso.
Mkutano
wa leo ulitanguliwa na mikutano miwili ambayo ilianza tarehe 11 hadi 14
Oktoba 2019, jijini Brazzaville ambapo pamoja na mambo mengine
ilijadiliwa suala la ugonjwa wa ebola na hali ya amani katika maeneo
yenye mlipuko wa ugonjwa huo.
Nchi
wanachama wa ukanda wa maziwa makuu ni pamoja na Angola, Burundi,
Jamhuri ya Kati, Demokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Kenya, Rwanda,
Sudan, Sudani Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.
Mwezi
Augusti, 2019 Umoja wa Maendeleo ya Nchi za Ukanda wa Kusini mwa Africa
(SADC) ulifanyika Tanzania Jijini Dar es Salaam nchi wananchama
waliridhia na kuipitisha kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ya Umoja huo
baada ya Kiingereza, Kireno na Kifaransa.
No comments:
Post a Comment