Na Irene Mark, Tabora
Mkuu wa shule ya Sekondary Tabora Wavulana, Deograsias Mwambuzi amesema wanatarajia kutumia historia ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa kitega uchumi cha shule hiyo.
Akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali waliotembelea shule hiyo aliyosoma hayati baba wa taifa alisema wameona fursa hiyo kutokana idadi kubwa ya wageni wanaotembelea shule hiyo kujifunza historia ya Mwalimu Nyerere.

Wanahabari hao na baadhi ya maofisa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia, wapo kwenye ziara ya kutembelea shule alizosoma na
kufundisha hayati baba wa taifa, Mwalimu Nyerere wakati taifa
likiadhimisha miaka 20 baada ya kifo chake na kuhakikisha historia yake
kwenye elimu inahifadhiwa vema.
Alisema taratibu za kuifanya makumbusho hiyo ya baba wa taifa kuwa sehemu ya kitega uchumi zimeanza kwa kumshirikisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

Mkuu huyo wa shule alisema baada ya Serikali kupitia Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia kufanya makumbusho makubwa katika shule hiyo
yameongeza hamasa ya wageni kutembelea shule hiyo na kujifunza historia
ya kinara wa harakati za ukombozi wa Tanganyika na Tanzania.
"Naishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi ma Teknolojia wametusidia kuboresha vyumba 17 vya madarasa, chumba cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Ofisi 10 za walimu, vyoo 15 na maktaba moja mpya

"...Maboresho hayo pia yalihusisha mfumo wote wa umeme na uondoaji wa
maji ya mvua ndio maana leo unaona mazingira ya shule yetu ni mazuri,"
alisema Mwalimu Mwambuzi.
Alisema shule ya Tabora iliwekwa jiwe la msingi mwaka 1922 na kuanza kazi mwaka 1925 hivyo ni shule yenye historia kubwa kwa nchi kwa kuwa viongozi wengi waliopambania uhuru walisoma hapo.

"Wakuu wa mihimili mitatu ya dola wamesoma hapa, Waziri Mkuu na baadae
Rais wa kwanza wa Tanganyika, Mwalimu Nyerere ametoka hapa, Spika wa
kwanza wa Bunge, Adam Sapi Mkwawa alikuwa hapa na hata Jaji Mkuu wa
kwanza pia alisoma Tabora school.
"...Mawaziri, wabunge na majaji wengi walisoma hapa kwa hiyo shule hii ni kisima na chimbuko la viongozi wa taifa hili na bado tunaendelea kupika viongozi hapa," alisema Mwalimu Mwambuzi.

Kwa mujibu wa historia ya shule ya Tabora, watoto wa watalala wa Uingereza na machifu wa Tanganyika ndio pekee waliosoma shule hiyo.
"Watoto wa wakoloni na machifu hii ndio ilikuwa shule yao na iliitwa Tabora school licha ya kuwa na upande wa wavulana na wasichana. Baada ya Serikali kuichukua kutoka kwa wakoloni ilipofika mwaka 1990 ikaitwa Tabora wavulana na ile nyingine ikaitwa Tabora wasichana," alisisitiza mkuu huyo wa shule ya Tabora wavulana.
No comments:
Post a Comment