Na Judith Mhina-Maelezo
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametoa funzo
kubwa kwa Watanzania kuwa tunahitaji kuwatengeneza watumishi aina ya
Rais Magufuli ili Tanzania iweze kusonga mbele.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli |
Sio
mara moja wala mbili Rais Magufuli amekuwa akijiuliza maswali kadhaa
kutokana na utendaji anaokutana nao katika ziara zake mikoani, na hatma
ya Tanzania huko tunakoelekea. Hii ina maana kubwa kwetu na ni vema
kupata majibu hayo kwa mstakabali wa Taifa letu.
Rais
Magufuli amekuwa akijiuliza maswali kadhaa ambayo mimi na wewe kutoa
majibu kwa haraka itakuwa ni uongo. Bali kama Watanzania tunawajibu wa
kumuahidi Rais kuwa kutokana na utendaji wake uliotukuka, tumeona
kinachojiri kwa sasa hapa Tanzania kwa kweli maendeleo makubwa
yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana ni wajibu kuwatengeneza
Magufuli wengi kwa mstakabali wa Taifa letu.
Baadhi
ya maswali hayo ambayo kila uchweo, katika ziara zake mikoani au wakati
za kuapisha viongozi mbalimbali Rais Magufuli anajiuliza na anasema
“Je nikiondoka leo Bwawa la Umeme la Nyerere litajengwa? Nikiondoka leo
reli ya kisasa (SGR) itajengwa Je Nikiondoka leo ndege zitanunuliwa?
Hapa ndipo napata nguvu ya kufanya kazi.”
Rais
Magufuli nguvu anayoipata kwa ajili ya kutimiza azma yake katika kuleta
maendeleo Tanzania, ndipo anapochochea azma ya vijana na watanzania
wenye uchungu na nchi hii kufikiri na kutafakari kwa nini na wao wasiwe
watendaji wazuri kama Rais Magufuli?.
Maneno
ya uchungu anayojiuliza Rais Magufuli yawe chachu kwa vijana
kutafakari na kuahidi kila mmoja nitaifanyia nini Tanzania. Kila kijana
wa Tanzania ajiwekee mikakati yake binafsi kwa kuangalia mifano hai ya
utendaji wa Rais Magufuli na kuahidi kufanya vema akiwa katika sekta
binafsi hapo alipo au sekta ya Umma.
Kitabu
cha Uongozi na Hatma ya Taifa la Tanzania cha Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere kimeeleza wazi aina ya kiongozi anayepashwa
kuiongoza Tanzania. Aidha miko na taratibu za uongozi ni lazima zifuatwe
ili kuhakikisha ustawi wa Taifa lolote lile duniani.
Kwanza
Rushwa ni Adui wa Haki suintatoa wala kupokea rushwa tuwatengeneza
vijana ambao wana nia ya dhati na dhamira zao zinatuambia kwake hakika
rushwa ni adui wahaki. Sifa hii Rais Magufuli ameidhibitisha kuwa
ameipiga vita rushwa kwa nguvu zote, hususan kupambana na watu wenye
fedha au kipato cha juu, Hakika kwa hili hongera na pongezi unastahili.
Vita
dhidi ya madawa ya lulevya, ambayo ni vita kali sana duniani kwa kuwa
wahusika wana uwezo wa kutoa rushwa ya kiasi chochote kilecha fedha,
kwa serikali na watendaji wake. Lakini Rais Magufuli amefanikiwa
kuimarisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa- TAKUKURU.
Pia,
kuanzisha Tume ya Kuratibu Uthibiti wa Dawa za Kulevya –Drug Control
Commission of Tanzania, ikiwa na kujitolea kwa vijana shupavu kama na wa
mfano kama, Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam Mhe. Paul Makonda, hiki ni
kithibitisho vijana wakuendeleza unayoaanza wapo.
Baba
wa Taifa amesema Rais tumtakaye ni yule ambaye anaweza kutetea Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar na kuhakikisha unadumu milele. Kwani ndio
kielelezo cha Umoja wetu, Amani Upendo na Mshikamano, ambao ndio dira
yetu na tunu ya Taifa letu.
Rais
Magufuli ni kiongozi ambaye ameonesha kielelezo hicho kwa uwazi na
kuahidi kuudumisha Muungano huo, kwa nguvu zake zote akili na maarifa
aliyojaliwa na Mwenyezi Mungu. Nina hakika wapo vijana ambao wanautetea
Muungano huu na kuenzi kwa nguvu akili maarifa na moyo wao wote.
Mfano
wa mambo yanayoimarisha Muungano ni uwepo wa Wizara za Muungano ambao
unafahamika, lakini wapo mawaziri kutoka upande wa pili wa Muungano
ambao wanashika nyadhifa ambazo sio wizara za Muungano, ikiwemo masuala
ya msamaha wa deni la Tanesco kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kiongozi
tumtakaye ni lazima aone nyufa za Muungano na awe na uwezo wa kuziba
nyufa hizo kabla hazijaleta madhara. Rais Magufuli amelidhibitisha hilo
na nachukua kila hatua ya kuhakikisha Muungano wetu unakuwa imara zaidi
kuliko wakati wowote .
Baba
wa Taifa amesema Tanzania inataka Rais ambaye atakuwa Mtumishi na sio
Mtawala, kiongozi anayeumizwa na shida na mahangaiko ya Watanzania.
Rais Magufuli amethibitisha hili kwa kusema sipo radhi kuongoza
Watanzania wanaotoa machozi. Rais anahangaika usiku na mchana
kuhakikisha anatatua shida na mahangaiko mbalimbali ya Watanzania.
Tumeshuhudia
Rais akichukizwa na ulanguzi wa korosho za wakulima na kuingilia kati
ili wasidhulumiwe jasho lao, lakini pia kujua haki zao kama wakulima.
Amechukizwa na ufujaji wa fedha za Umma kwenye sherehe ambazo hazina
tija na kuzipeleka kufanya usafi wa mazingira na kupambana na ugonjwa
wa kipindupindu na kununua dawa.
Serikali
ya Awamu ya Tano inakusanya kodi kwa kila mtu bila ubaguzi, kwa mara ya
kwanza katika historia ya nchi imevunja rekodi ya kukusanya fedha za
Tanzania Trilioni 1.8 kwa mwezi Agosti 2019. Nyerere alisema katika
moja ya hotuba zake serikali corrupt haikusanyi kodi, inabaki
kukimbizana na wafanya biashara wadogo wadogo.
Rais
Magufuli ameumwa na mahangaiko ya wafanyabiashara ndogondogo
(wamachinga ) amekuja na mfumo madhubuti ya kuwafanyia wafanye biashara
zao kwa uhakika zaidi bila kubughudhiwa. Kuanzishwa kwa vitambulisho
maalum vya Rais ndio kielelezo cha kuonyesha ni jinsi gani anaumizwa na
mahangaiko ya watanzania.
Rais
tumtakaye ni yule anayeweza kuwa mbunifu kutokana na rasilimali
tulizonazo na kuhakikisha Taifa linajitegemea ili kuleta heshima. Rais
Magufuli amelitekeleza kwa kutumia fedha za ndani katika kujiletea
maendeleo, sasa nchi inaheshimika ukikataa na fedha zako haijalishi
nchi inasonga mbele. Vijana wanaona Rais anavyofanya wanajifunza
wanakuelewa kwa kuwa wazalendo wapo.
Kuanzishwa
kwa sera ya Elimu bure Tanzania kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato
cha nne kila mwezi serikali inatoa jumla ya Bilioni 23. 5 kwa ajili ya
Elimu bure shule za sekondari na za Msingi Tanzania Bara.
Kwa
sasa kuna vijana wengi sana ambao wapo shule na hawahangaiki tena na
kukimbizana na Walimu, Wazazi wafadhili na wengineo katika kutafuta
fedha za ada. Matokeo yake hata watoto wa maskini kwa sasa wapo shule.
Ndio hao hao watakaokuja kuchukua nafasi za uongozi katika nchi hii na
hakika tutambue vijana wanaona anachofanya Rais Magufuli.
Tumeshuhudia
miaka mingi inapita migogoro ya ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji,
Wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi ikiwemo hifadhi za Taifa. Rais
Magufuli hili limemuuma Sana na kuhakikisha jumla ya vijiji 920 kati ya
975 nchini vilivyopo maeneo ya hifadhi vimetambuliwa rasmi. Yote haya
kwa masilahi ya watanzania wanyonge vijana wanaona nina hakika watafata
nyayo zako.
Aidha,
Tanzania imefuta maeneo ya akiba 12 yenye ekari 707, 659, 95 na misitu 7
yenye ekari 46,715. Pia serikali imeamua kumega eneo la hifadhi 14 ili
kuwapa wananchi maeneo ya kuishi kuzalisha kilimo na ufugaji ambapo
katika uamuzi huo vijiji 60 vinavyonufaika ni vya Mkoa wa Katavi.
Kiongozi
bora ni yule anaweza kutoa suluhisho la kudumu kwa watu wanaohusika
badala ya kubaki na ngonjera za utafiti unafanywa, tupeni muda serikali
inalifanyia kazi, nimeagiza viongozi watatoa mustakabali wa tatizo
hilo. Utasikia mchakato unaendelea miaka nenda miaka rudi.
Kitabu
cha Uongozi wa Tanzania na Hatma yake cha Baba wa Taifa Nyerere
kinasema Rais tumtakaye ni yule anayeguswa na matatizo ya majirani zake
Rais Magufuli ameonyesha Mfano wa kuhakikisha majirani zake waliopata
dhoruba ya kimbunga cha Kenneth kilichotokea mapema mwezi April 2019 na
kuadhiri Malawi, Msumbiji, Zimbabwe, na kuhakikisha Tanzania inatoa
msaada wa tani za mahuindi kadhaa kwa Malawi Zimbabwe na Msumbiji.
Jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa Afrika –SADC kwa sasa imepamba moto na nchi ya
Tanzania ndio Mwenyekiti, ambapo imeonyesha dira kwa kuzindua Kituo cha
Huduma za Pamoja za Mpakani, Nakonde One Stop Post ili kuongeza
mtengamano wa Jumuiya hiyo katika masuala mbalimbali ya Bishara,
Mawasiliano, Uchukuzi na mengineyo.
Rais
wa Tanzania awe ni yule anayetaka kuwaletea maendeleo watanzania sio
kujiletea maendeleo yeye mwenyewe, familia yake na marafiki zake. Rais
magufuli ametia fora katika eneo hilo barabara nyingi zimejengwa nchi
nzima kwa kiwango cha lami, barabara hizi ni kichocheo kikubwa cha
uchumi, Rais Magufuli vijana wanaona na kuona ni kuamini.
Vituo
vya Afya 320 Zahanati na Hospitali za Wilaya kadhaa za Rufaa Mkoa
zimejengwa na kuimarishwa, Bajeti ya dawa imeongezwa na dawa
zinapatikana hospitali zote za serikali kutoka Bilioni 32 mpaka Bilioni
352. Vyumba vya madarasa vingi vimejengwa ndani ya miaka mitatu ya
uongozi wa Awamu ya Tano.
Rais
tumtakaye ni yule anayehimiza Umoja Mshikamano Upendo kwa Watanzania na
ndio maana Tanzania na ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
imetengemaa, uanzishwaji wa Umoja wa forodha katika mipaka ya Tanzania
na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.
Aidha,
Ushirikiano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika –SADC ni
kielelezo kingine ambacho kinaonyesha Tanzania imeadhimia kuhakikisha
dhamira ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ya Umoja wa Afrika inatimizwa.
Rais
tumtakaye ni yule asiye na ubaguzi wa dini, rangi sura eneo atokalo mtu
kabila au vinginevyo. Watanzania wote ni sawa na Afrika ni moja Rais
Magufuli anasema “Naomba mniombee nisibadilike niwatumikie Watanzania
kwa moyo wangu wote akili na maarifa, naomba nisibadilike nisiwabague
Watanzania kwa kabila zao, dini zao, rangi zao maeneo wanayotoka naomba
mungu anisaidie”
Rais
Magufuli amesema “Siwezi kuendesha nchi ambayo watu wake wanatoa
machozi” Viongozi wetu wametimiza wajibu wao, uamuzi ni wa Watanzania
kuamua kutumikia nchi yao kwa nidhamu na heshima, upendo na amani kila
utendalo liwe kwa masilahi ya nchi na sio vinginevyo. Rais magufuli
matendo yako yatatengeneza MAGUFULI WENGI WAJAO MUNGU IBARIKI
TANZANIA.
No comments:
Post a Comment