Timu
ya Madereva kutoka Uingereza ikipanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la
kuchangisha fedha kwa ajili ya maveterani wa kijeshi (military veterans)
huko Uingereza.
Timu
ya madereva taxi watano kutoka Uingereza ilifanya ziara nchini kuanzia
tarehe 28 Septemba hadi 10 Oktoba 2019. Ziara hiyo iliratibiwa na Wizara
kupitia Ubalozi wetu London kwa kushirikiana na TTB. Timu hiyo ilikuja
nchini kwa ajili ya kupanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni zoezi la hisani
ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maveterani wa kijeshi (military
veterans) huko Uingereza.
Timu ya Madereva wa Taxi kutoka Uingereza ikiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro (Uhuru Peak).
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo akitoa neno katika hafla ya uwekaji
saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB) na Timu ya Madereva wa taxi watano kutoka Uingereza. Makubaliano
hayo yalihusu timu ya madereva wa Uingereza kuwa Mabalozi wa hiari wa
kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uingereza.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Sarah Cooke akizungumza katika hafla hiyo
Katika
kutambua uamuzi mzuri wa timu hiyo kuuchagua mlima Kilimanjaro kwa
zoezi hilo la hisani na kwa malengo ya kunufaika na ujio wao katika
kutangaza vivutio vyetu vya utalii nchini Uingereza, Wizara ya Mambo ya
Nje kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iliwaandalia timu
hiyo ziara ya kutembelea vivutio vya utalii mbalimbali hapa nchini
zikiwemo mbuga za wanyama za Serengeti, Ngorongoro na Tarangire.
Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Dkt. Devota Mdachi na Kiongozi wa Madereva wa Taxi wakiweka saini MoU
Vilevile,
Timu hiyo ya madereva taxi baada ya kumaliza kutembelea vivutio
vilivyotajwa hapo juu walitangazwa kuwa mabalozi wa hiari wa utalii
(tourism goodwill ambassadors) wa Tanzania kwa lengo la kutangaza
vivutio vya utalii vya hapa nchini wawapo katika shughuli zao huko
Uingereza. Hafla ya kuwatangaza ilifanyika Hotel ya Mount Meru Arusha.
Baada ya kutangazwa kuwa mabalozi wa hiari, walisaini Hati ya
Makubaliano (MoU) kati ya timu hiyo na TTB tayari kwa kutekeleza
majukumu yao.
Hati ya Makubaliano baada ya kusainiwa ikioneshwa kwa wajumbe walioshiriki hafla ya uwekaji saini.
Madereva wa Taxi, baadhi yao wakiwa na wenza wao baada ya hafla ya uwekezaji saini MoU
Tukio
hilo lilihudhuliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya maliasili na Utalii
Dkt. Aloyce Nzuki, akimuwakilisha Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangallah (Mb),
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo. Aidha, Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Balozi wa
Uingereza hapa nchini, Mhe. Sarah Cooke.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
No comments:
Post a Comment