|
Naibu Waziri wa Uchukuzi
na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa
Vodacom, Benedict Mara (wa kwanza kulia) kuhakikisha mawasiliano yanapatikana
muda wote Kata ya Ilolangulu wakati wa zaiara yake ya kukagua upatikanaji wa
hudumaza mawasiliano wilayani Mbogwe, Geita
Naibu Waziri wa Uchukuzi
na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye yuko ziarani mkoani Geita kukagua
upatikanaji wa huduma za mawasiliano, kuhamasisha wananchi kusajili laini za simu
kwa njia ya alama ya vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA na
kufuatilia utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi mkoani humo
Wakati akiwa kwenye
ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Mbogwe, Nditiye amesema kuwa malengo ya Serikali ni
kuhakikisha kuwa wananchi wanawasiliana, huduma za mawasiliano zinakuwa zenye
ubora unaotakiwa, za uhakika na kunakuwa na usikivu mzuri wa mawasiliano kwa
kuwa Serikali inataka wananchi wawasiliane
“Serikali tunataka
wananchi wawasiliane kwa kuwa wakiwasiliana tunapata mapato ambayo yanaendesha
shughuli mbali mbali za kuhudumia wananchi,” amesema Nditiye
Mkuu wa Wilaya ya
Mbogwe, Martha Mkupasi amemweleza Nditiye kuwa wanashida ya mawasiliano kwenye
wilaya yao na mara nyingine wanakwama kukusanya mapato ya Serikali hivyo
inawapa changamoto katika kuwatumikia wananchi na utekelezaji wa majukumu ya
kila siku ya Serikali
|
|
Mkuu
wa uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard akitoa
taarifa kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye
(wa kwanza kushoto) kuhusu mnara wa Ilolangulu wakati wa ziara yake ya kukagua
upatikanaji wa mawasiliano Mbogwe mkoani Geita |
|
|
Mbunge wa jimbo la
Mbogwe, Agostino Masele akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Atashasta Nditiye vijiji ambavyo havina mawasiliano ya uhakika wakati wa ziara
yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano wilayani Mbogwe mkoani Geita
|
|
Mkuu wa Wilaya ya
Mbogwe, Martha Mkupasi akitoa taarifa ya hali ya mawasiliano kwa Naibu Waziri
wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake
wilayani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano
|
“tunashida ya
mawasiliano kwenye wilaya yetu na mara nyingine tunakwama hata kukusanya mapato
na kupeana taarifa za ulinzi na usalama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi,” amefafanua Mkupasi
Nditiye amemweleza kuwa
amekagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano wilayani humo na amegundua kuwa
Wilaya ya Mbogwe inapata mawasiliano kwa kiwango cha asilimia 90 na ina mitandao
mingine ya mawasiliano ila wananchi wanaonekana wanapenda mtandao wa Vodacom
Naye Mbunge wa Mbogwe,
Agostino Maselle amekiri kuwa wanapata huduma za mawasiliano za mitandao
mingine ya TTCL, tigo, halotel, airtel na yote iko vizuri ila mtandao wa
Vodacom unasumbua na huduma za m-pesa kwenye kata ya Ilolangulu, Itobe na
Isesya
Akizungumza kwa niaba ya
wananchi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kata ya Ilolangulu, mkazi wa kata
hiyo Daniel Mishigitu amemweleza Nditiye kuwa wanapata kero ya mawasiliano ya
Vodacom na wakitumiwa hela inakaa muda mrefu kwenye mtandao. Naye Vedastus
Rwechungura amemshukuru Nditiye kwa kufika na kusikiliza shida ya mtandao huo
na mzunguko wanaoupata wakitaka kutoa pesa ambapo mara nyingine wanalazimika
kusafiri kwenda Ushirombo
Akijibu malalamiko ya
wananchi, Nditiye amewaeleza kuwa amegundua kuwa kuna mzunguko wa hela kwenye
kata hiyo na uchumi wa wananchi uko vizuri, hivyo ameielekeza kampuni ya
Vodacom kuwa ndani ya muda wa miezi sita mnara uwepo ili wananchi waweze
kuwasiliana, kutuma na kupokea pesa kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha
wananchi wanawasiliana na wakiwasiliana inapata mapato
Nditiye amefanunua kuwa
sehemu inapokuwa na mawasiliano ya kampuni moja inatosha na sio lazima kuwa na
mitandao yote ila kwa kuzingatia kuwa wananchi wamehitaji mtandao huo hivyo
UCSAF kwa kushirikiana na Vodacom ihakikishe kuwa mnara huo unajengwa na TCRA
wafuatilie na kusimamia jambo hilo
Katika ziara hiyo,
Nditiye ameambatana na wataalam kutoka wizarani kwake Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na
watoa huduma wa kampuni ya VodacomPrisca
Ulomi, Geita
No comments:
Post a Comment