|
Naibu Waziri wa Uchukuzi
na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akiielekeza kampuni ya Vodacom
kuhamisha mnara na ujengwe eneo la shule ili kuepusha mgogoro na mmiliki wa
eneo ulipojengwa mnara huo wakati wa ziara yake kwenye mnara huo, kijiji cha
Bukuku, kata ya Rufita wilayani Nyang’hwale, Geita
|
Naibu Waziri wa Uchukuzi
na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ameielekeza kampuni ya simu ya
Vodacom kuhamisha mnara wake uliopo kijijii cha Bukuku, Kata ya Kafita wilayani
Nyang’hwale mkoani Geita ili kumaliza mgororo uliopo baina ya Serikali na
mwananhi anayemiliki eneo ulipojengwa mnara huo na kuujenga kwenye eneo la
shule ya Msingi kulumbai iliyopo karibu na mnara huo ili wananchi wa kata hiyo
waendelee kupata za mawasiliano
Nditiye amtoa maelekezo
hayo alipofika kwenye eneo la kijiji cha Bukuku ulipojengwa mnara huo wakati wa
ziara yake wilayani Nyang’hwale ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwa
wananchi na kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Hamim Guyama kuwa mmiliki wa eneo hilo Bi.
Rukia Kashokelo na mme wake Clement Fungameza amekataa kusaini mkataba wa
Vodacom na ameridhia mnara huo ung’olewe
“Mnara huu kwa huyu mama
uhame tu kwa kuwa upo kwenye jiwe na anataka alipwe shilingi mioni kumi kwa
mwaka na anakosesha mawasiliano, amegoma kupokea shilingi milioni mbili na laki
nne kwa mwaka na eneo hili kuna migodi mitatu na mapato ya takribani bilioni 20
kwa mwaka na ni eneo linalohitaji mawasiliano kwa uchumi na ulinzi na usalama
wa kata ya Kafita,” amesema Guyama
|
Naibu Waziri wa Uchukuzi
na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akipata maelezo ya mgogoro wa mnara
kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji cha Bukuku kilichopo kata ya Kafita, Nyang’hwale
mkoani Geita, Eunice Gombanila wakati wa ziara yake kwenye eneo ulipojengwa
mnara huo
|
Guyama amefafanua kuwa
mmiliki wa eneo amefanya jitihada za kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ili kuhakikisha kuwa wanapata malipo hayo
kwa kukodisha eneo lao ulipojengwa mnara na kukataa kusaini mkataba na Vodacom
wa malipo ya awali waliyokubaliana
Nditiye ameipata kampuni
ya simu ya Vodacom kuhakikisha kuwa inahamisha mnara huo ndani ya mwezi mmoja
na amepiga marufuku kwa kampuni za simu zinazojenga minara kwa kutumia ruzuku
ya Serikali wanayopewa kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kujenga
mnara kwenye eneo la mtu binafsi ili kuepusha migogoro kwa kuwa Serikali haiko
tayari kuingia migogoro na wananhi wake bali minara ijenge kwenye maeneo
yanayomilikiwa na Serikali ya kijiji, shule au maeneo ya kanisa au misikiti ili
wananchi wanufaike na fedha zinazolipwa na kampuni za simu
|
Mkuu wa Wilaya ya
Nyang’hwale, Hamimu Guyama akitoa taarifa ya mgogoro wa mnara wa Kata ya Kafita
kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye
(katikati) wakati wa ziara yake wilayani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma
za mawasiliano. Wa kwanza kushoto ni mbunge wa jimbo hilo, Houssein Amir
|
Naye Mtendaji wa Kijiji
cha Bukuku kilichopo kata ya Rufita wilayani Nyag’hwale mkoani Geita, Eunice
Gombanila ulipojengwa mnara huo amemweleza Nditiye kuwa mama huyo amekataa
kupokea na kusaini mkataba baina yake na Vodacom ambapo alilazimika kukaa na
mkataba huo ofisini kwake kwa muda wa wiki nne bila ya mafanikio na alipomfuata
mmmiliki wa eneo hilo alikataa kusaini mkataba huo na maeridhia ung’olewe
Mkuu wa Uedeshaji wa
UCSAF, Mhandisi Albert Richard amesema kuwa ujenzi wa mnara huo umegharimu dola
za marekani 180,000 ambazo ni zaidi ya shiingi milioni 200 za kitanzania na
kuongeza kuwa mnara huo umehujumiwa kwa kung’olewa paneli tatu za sola ambazo
zinazalisha umeme wa jua kwa ajili ya kuwasha mnara huo ili uweze kuwaka na
kusambaza mawasiliano kwa wananchi
|
Naibu Waziri wa Uchukuzi
na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya
ya Nyang’hwale, Hamimu Guyama kitabu cha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote chenye
orodha ya minara iliyojengwa na Serikali wilayani humo wakati wa ziara yake ya
kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano.
Mhandisi wa Vodacom,
Benedict Mara ameishukuru Serikali kwa kutoa maelekezo ya kuhamisha mnara huo
na watatekeleza maelekezo hayo ili waweze kuendelea kutoa huduma za mawasiliano
kwa wananchi na wakazi wa kata ya Kafita
Mkuu wa Shule ya Msingi
ya Kulumbai iliyopo Kata ya Kafita wilayani Nyang’hwale, James Jacob amefurahia
uamuzi wa Serikali wa kujenga mnara huo kwenye eneo la shule baada ya mmiliki
wa eneo ulipojengwa mnara huo hapo awali kuridhia ung’olewe kwa kutaa malipo ya
Vodacom na amesema kuwa malipo hayo yataiwezesha shule kujiendesha
Mbunge wa Nyang’hwale,
Houssein Nassoro Amir amemweleza Nditiye kuwa anaiomba Serikali kuboresha
mawasiliano ya kata ya Nyamtukuza, Nundu, Nyijundu, Kafita, Kaboha na Shabaka
kwa kuwa kuna shida ya mawasiliano na ukitaka kupata taarifa saa tano asubuhi
unapata saa kumi jioni hivyo inaleta changamoto ya ulinzi na usalama
“Serikali inatumia
mtandao kukusanya mapato yake ila mtu analazimika kukaa na fedha kwa muda mrefu
kwa sababu usikivu wa mawasiliano sio mzuri hivyo tunashindwa kukusanya mapato
ya Serikali kwa wakati,” amesisitiza Amir
|
|
Mhandisi wa Kampuni ya
Vodacom, Benedict Marwa, akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) kwa niaba ya Serikali kwa
kuielekeza kuhamisha mnara wa kata ya Kafita ili kuepusha mgogoro na mmiliki wa
eneo wakati wa ziaa yake wilayani Nyang’hwale, Geita.
Katika hatua nyingine,
Nditiye amemwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),
Waziri Waziri Kindamba na Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta kufika wilayani
Nyang’hwale ndani ya mwezi huu wa Oktoba, 2019 na kufungua ofisi zao ili kuweza
kuwahudumia wananchi na kusogeza karibu huduma zao. Na
Prisca Ulomi, Nyang’hwale, Geita
|
No comments:
Post a Comment