Na Festo Sanga, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kigoma
Kamati
ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kigoma ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga imetembelea Jengo la
Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma na Nyumba za Makazi za Majaji na kupongeza
upatikanaji wa huduma ya Mahakama Kuu katika mkoa huo.
Ugeni
huo ulitembelea miradi hiyo ya ujenzi mapema Oktoba 08, 2019 na
ulipokelewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma Mhe. Jaji
Ilvin Mugeta.
Katika
ziara hiyo, Brigedia Jenerali Mstaafu Maganga amepongeza jitihada za
Mahakama ya Tanzania katika kusogeza huduma kwa wananchi wa Mkoa wa
Kigoma kwani awali walikuwa wakisafiri umbali wa takribani kilomita
858(kwenda na kurudi) kufuata huduma za Mahakama Kuu Mkoani Tabora.
Pia
amepongeza utendaji kazi wa Mkandarasi wa ‘Masasi Construction Co
Ltd’ anayejenga jengo la Mahakama Kuu pamoja na nyumba za Makazi za
Majaji.
“Wajumbe
wenzangu tuone uwezekano wa kuwatumia wakandarasi hawa katika miradi ya
ujenzi kutokana na kazi waliyoifanya katika jengo hili,” alisema Mkuu
wa Mkoa
Ziara
hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa Mpango ulioandaliwa na Uongozi wa
Mahakama Kuu Kigoma kuhakikisha wadau wa Mahakama Mkoa wa Kigoma
wanapata fursa ya kutembelea jengo hilo jipya na kujionea miundo mbinu
iliyopo ikiwa ni pamoja na kupata elimu.
Baadhi
ya wadau wakiwemo wajumbe wa Haki Jinai Mkoa, wajumbe wa vituo vya
msaada wa kisheria( paralegal) Mkoa wa Kigoma, watumishi wa Mahakama
Kanda ya Kigoma, wazabuni mbalimbali waliweza kutembelea jengo hilo
ambalo linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga
(katikati) akifafanua jambo wakati yeye pamoja na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ilipofanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa Mahakama Kuu
Kigoma na nyumba za makazi ya Wahe. Majaji.
Muonekano wa jengo jipya la Mahakama Kuu, Kanda ya Kigoma.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma Mhe. Jaji Ilvin Mugeta
akiongoza msafara wa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi mara walipofika Katika
jengo la Mahakama Kuu Kigoma. Nyuma ya Mhe. Jaji ni Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga akiteta
jambo na Mhe. Jaji Mfawidhi pamoja na Wakandarasi katika UKumbi wa Wazi
wa Jengo la Mahakama Kuu.
Picha ya pamoja ya Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kigoma, Viongozi wa Mahakama na Wakandarasi wa 'Masasi Construction Ltd.'
No comments:
Post a Comment