Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan
Abbasi, jana jioni alilazimika kumpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hoseah Kashimba
ili kutatua kero za walimu waliodai kuna wenzao wamestaafu hawajalipwa
mafao yao.
Tukio
hilo lilijitokeza wakati Dkt. Abbasi akijibu hoja za walimu mara baaya
ya kuwasilisha mada wakati wa Mkutano ulioandaliwa na Chama cha Walimu
Tanzania (CWT) mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na walimu kutoka mikoa ya
Kigoma, Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera
Katika mkutano huo walimu walitaka kujua ni lini Serikali italipa pesheni kwa wastaafu ambao hawajalipwa kwa muda mrefu.
Dkt.
Abbasi alionesha kushangazwa na hali hiyo kwani aliwaeleza wanasemina
hao kuwa Serikali imeachana na utamaduni wa zamani wa kulimbikiza madeni yasiyo na sababu.
Alitoa
mfano kuwa licha ya TZS Bilioni zaidi ya 40 zilozotolewa mwaka 2017
kulipa madeni ya wastaafu, Serikali pia ilihakikisha
kati ya hizo TZS Bilioni 16 zinahusu walimu.
Akaongeza
kuwa hata mwaka huu kati ya Julai na Septemba Serikali imelipa madeni
yanayofikia TZS Bilioni 85.62 ambapo kati ya hizo TZS Bilioni 50 ni
madai ya pensheni, Bilioni 22 ni madai mbalimbali ya watumishi wa umma
na nyingine ni wadai wa sekta binafsi.
Kutokana
na madai ya kuwepo wastaafu wa kada ya elimu ambao hawajalipwa muda
mrefu, baadhi wakidai kuwa ni mwaka mzima, Dkt. Abbasi alimpigia simu na
kumuunganusha moja kwa moja kwenye kipaza sauti Mkurugenzi Mkuu wa
PSSSF.
Akijibu
hoja hiyo, Bw. Kashimba alisema kuwa Serikali kupitia PSSSF
imeendelea kuwalipa pensheni wastaafu wote kwa wakati na kutoa ofa kwa
mwalimu yeyote ambaye hajalipwa kwa muda mrefu alete vielelezo suala
lake litafanyiwakazi haraka.
“Mmesikia
wenyewe, kama nilivyosema, Serikali ya Rais Magufuli ni ya kisayansi.
Hili sasa limekwisha, sio kulalamika tena lete ushahidi wa majina na
namba ya malipo ya mishahara ya mtumishi husika, suala lake litatatuliwa
haraka,” alisema Dkt. Abbasi kuwaeleza walimu hao waliokuwa na furaha
tele baada ya ofa ya Mkurugenzi wa PSSSF.
Baadhi ya walimu hawakuwa na vielelezo husika lakini wachache waliwasilisha nyaraka zao na zinafanyiwa kazi.
Dkt.
Abbasi amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Mkoa wa Simiyu,
ambapo awali aliudhuria hafla ya kufunga Kambi za Kitaaluma kwa
Wanafunzi wa Kidato cha Nne katika mwaka 2019.
Na Immaculate Makilika- MAELEZO
No comments:
Post a Comment