Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Beng'i Issa akizungumza wakati wa mafunzo hayo |
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya kazi,Vijana na ajira Anthony Mavunde akizungumza wakati wa akifunga mafunzo ya ujasiriamali kwa Vijana yaliyofanyika mkoani Tanga |
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo
Serikali
imesema itahakikisha inaendelea kuliwezesha kwa ujuzi kundi la Vijana
ili waweze kushiriki kwa vitendo katika shughuli za kiuchumi na ujenzi
wa Taifa
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
masuala ya kazi,Vijana na ajira Anthony Mavunde Leo wakati wa kufunga
mafunzo ya ujasiriamali kwa Vijana yaliyofanyika mkoani Tanga
Alisema
kuwa kwa mujibu wa utafiti wa nguvu kazi wa mwaka 2014 inaonyesha kuwa
ukosefu wa ajira kwa Vijana ni asilimia 11.7% duniani ambapo kitaifa ni
asilimia 10.3%.
Hivyo
kutokana na changamoto hiyo serikali imeweza kuja na mikakati endelevu
ya kuliwezesha kundi Hilo kupata ujuzi wa kushiriki katika shughuli za
uzalishaji mali kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa.
"Tunatambua
kwamba kikwazo kikubwa kwa Vijana kushindwa kunufaika na fursa hasa za
miradi ya kimkakati ni kutokuwa na ujuzi stahiki ,hivyo kwa mafunzo hayo
Nina imani yatakwenda kumaliza changamoto ya ajira nchini"alisema Naibu
Waziri Mavunde.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi
kiuchumi Beng'i Issa alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa vijana
kwani wanayahitaji kwa kutambua kuwa ujuzi ndio msingi mkubwa wa
maendeleo.
Alisema
kuwa mafunzo hayo yatawaongezea ubunifu na kutatua changamoto
wanazokutana nazo katika shughuli mbalimbali za kiuchumi wanazozifanya.
Mpaka Sasa jumla ya vijana 1,222 wamenufaika na mafunzo hayo katika mikoa ya Dodoma,Ruvuma,Geita, Mwanza, Mbeya, Lindi na Tanga
No comments:
Post a Comment