Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masula ya Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia
vijana wakati wa mdahalo wa miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl.
Julius Kambarage Nyerere uliofanyika kwenye ukumbi wa Sea View, Mkoani
Lindi.
Baadhi
ya Vijana wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masula ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mdahalo wa miaka
20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere
uliofanyika Mkoani Lindi.Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza wakati wa mdahalo huo.
Sehemu
ya viongozi wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa
mdahalo wa miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage
Nyerere uliofanyika kwenye ukumbi wa Sea View, Mkoani Lindi. Katikati ni
Katibu Mkuu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally.
Mama Gertrude Mongela akiwasilisha mada kuhusu Miaka 20 bila Baba wa Taifa wakati wa mdahalo huo uliofanyika Mkoani Lindi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masula ya Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akifuatilia
mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mama Gertrude Mongela kuhusu Miaka 20
bila Baba wa Taifa wakati wa mdahalo huo. (Wa pili kutoka kushoto) ni
Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Abeid
Karume na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira)
Mhe. Anthony Mavunde. Kulia ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis
Mutungi.
Baadhi
ya washiriki kwenye mdahalo huo wakifuatailia mada zilizokuwa
zinawasilishwa. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania
(TBC) Dkt. Ayub Rioba. (Wa pili kutoka Kushoto ni Mjukuu wa Mwalimu
Julius Kambarage NyerereMjukuu
wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bi. Ngusekera Nyerere akitoa salamu
wakati wa mdahalo huo wa kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa
Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika Mkoani Lindi.
Wawasilishaji
Mada wakisikiliza hoja zilizokuwa zikichangiwa na baadhi ya washiriki
wakati wa mdahalo huo wa kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa
Mwl. Julius Kambarage Nyerere uliofanyika kwenye ukumbi wa Sea View,
Mkoani Lindi.
Kijana mmoja wapo aliyeshiriki mdahalo huo akichangia mada kuhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka
vijana nchini kuenzi na kuziishi fikra na mitazamo za Baba wa Taifa,
Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuendeleza umoja uliopo nchini.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Mkoani
Lindi Oktoba 13, 2019, Waziri Mhagama alisema kuwa vijana wanapaswa
kuendeleza mambo mema yote aliyoyafanya Baba wa Taifa enzi za uhai wake
ili waendelee kujivunia juu ya misingi ya amani na umoja iliyopo nchini.
“Vijana
mna kila sababu ya kujivunia amani na umoja ulipo katika taifa letu kwa
kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi aliyewapenda watu wote bila
kujali imani zao wala itikadi zao, alikuwa mzalendo na alitaka
watanzania wote waishi kwa umoja,” alisema Mhagama.
Aidha
alifafanua kuwa, Amani na umoja zilikuwa ni miongoni mwa tunu na falsafa
kuu za Baba wa Taifa ambayo ndiyo matokeo ya umoja na mshikamano wa
taifa uliopo sasa.
Aliongeza
kuwa miongoni mwa mambo muhimu ambayo Baba wa Taifa alikuwa akisisitiza
katika kuwaunganisha watanzania ni pamoja na kulijengea uhuru taifa na
watu watu wake, kudumisha amani, upendo, umoja, uzalendo, mshikamano na
kuandaa sera za kukabiliana na ujinga, umaskini na maradhi.
Pamoja
na hayo alisisitiza pia vijana na wananchi kumuunga mkono Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kazi kubwa anayoifanya kuendeleza maono ya Baba wa Taifa ikiwemo mageuzi
ya kiuchumi yenye manufaa kwa taifa.
Akitolea
mfano sekta ya elimu ambayo serikali ya awamu ya tano imekuwa ikitoa
elimu bure ilikuwa ni falsafa ya Mwalimu katika kuwajenga watanzania
fikra ya kujitegemea ili waweze kuukabili umasikini.
Waziri
Mhagama alitumia fursa hiyo pia kuwahimiza wananchi kuendeleza maudhui
ya Mwenge wa uhuru ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwaunganisha
watanzania na kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee
maendeleo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi alisema kuwa
Mwalimu Julius Nyerere ataendelea kukumbukwa na Watanzania kwa mchango
wake aliojitolea katika kulijenga taifa.
No comments:
Post a Comment