Mkurugenzi
Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Raphael Waida (kulia) na mtaalam
wa uchambuzi wa masuala ya Utawala, Bi. Beltila Mgaya, wakifuatilia kwa
makini hoja za washiriki wa mafunzo ya maboresho ya Mkataba wa Huduma
kwa Wateja wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Arusha.
Wizara
ya Fedha na Mipango inaboresha Mkataba wa utoaji Huduma kwa wananchi
kwa kupata maoni katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma lengo likiwa
kuongeza ufanisi na kufikia maendeleo stahiki kwa wakati.
Hayo
yamebainishwa na Mchumi Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi.
Fortunata Soka, wakati wa mafunzo ya ukusanyaji wa maoni ya maboresho ya
Mkataba wa Huduma kwa Wateja kwa wadau wa Wizara hiyo yaliyofanyika
Jijini Arusha na kuwakutanisha wadau kutoka Wizara hiyo pamoja na Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Raphael Waida, akisisitiza
umuhimu wa kuwa na tabia ya kujali wateja, wakati wa mafunzo ya
maboresho ya mkataba wa huduma kwa wateja kwa Wizara ya Fedha na
Mipango, Jijini Arusha. Kushoto ni mtaalam wa uchambuzi wa masuala ya
Utawala, Bi. Beltila Mgaya
Bi.
Soka alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imekuwa na Mkakati wa
Utoaji huduma kwa wananchi ambao sasa unahitaji maboresho ili kuongeza
ufanisi wa huduma na kuharakisha maendeleo ya wananchi.
‘’Muundo
wa Wizara umebadilika na pia wadau wanaongezeka hivyo kuna kila sababu
ya kuboresha mkataba wa huduma kwa wateja ili kukidhi uhitaji,
tunalazimika kufanya mafunzo ya namna ya kufanya tafiti kwa wadau ili
kuja na mkataba bora uliosheheni weledi na kuleta matokeo chanya kwa
walengwa.’’, alieleza Bi. Soka
Alisema
kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua kwa kufikisha huduma kwa
haraka kwa wananchi hivyo Wizara inalengo la kupata mrejesho wa utoaji
wa huduma zake ili kuweza kuandaa mipango yenye manufaa kwa wananchi na
Taifa kwa ujumla
Mchumi
Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Fortunata Soka, akielezea
umuhimu wa kufanya maboresho ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Wizara
hiyo, wakati wa mafunzo ya maboresho ya mkataba huo, Jijini Arusha.
Bi
Soka alisema kuwa maboresho ya Mkataba wa huduma kwa wateja ni sehemu ya
kujali wananchi hasa wa hali ya chini ambao wanataka kupata huduma bora
kwa ufanisi kwa maendeleo yao kwa kupunguza urasimu usio wa lazima.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni
mtoa mada, Bw. Raphael Waida, alisema kuwa ili kuweza kutoa huduma bora
kwa wananchi lazima mikataba ya huduma kwa wateja ikafanyiwa maboresho
kila inapobidi kwa kuwa teknolojia na mazingira ya kihuduma
yanabadilika.
Mchumi
wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Henrico Ndagula (kushoto) akiomba
ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya mkataba wa huduma kwa wateja kwa
Wizara hiyo, wakati wa mafunzo ya maboresho ya mkataba huo, Jijini
Arusha.
Baadhi
ya Washiriki wa Mafunzo ya maboresho ya mkataba wa huduma kwa wateja
kwa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Arusha, wakisikiliza kwa makini
mada zilizokuwa zikiwasilishwa.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)
Aidha,
ameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa jitihada zake za kuhakikisha
inatoa huduma kwa wadau kwa wakati hasa katika kipindi hiki ambacho
Serikali imejidhatiti kufikia uchumi wa Kati uliojikita katika viwanda
kwa manufaa ya wananchi.
Naye
Mchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Henrico Ndagula ambaye ni mmoja
wa Washiriki wa Mafunzo amesema kuwa, mafunzo hayo yanasaidia kufanya
tathmini ya utoaji huduma na kuangalia maeneo ambayo Wizara imefanikiwa
na yanayohitaji maboresho, hivyo kuwa na umuhimu hasa katika wakati huu
ambao mabadiliko makubwa yakiuchumi yanafanyika nchini.
Na. Peter Haule, WFM, Arusha
No comments:
Post a Comment