Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akikata Utepe kuashiria
Uzinduzi wa Vitabu vya Sera ya Viwanda katika hafla ya Uzinduzi wa Sera
ya Viwanda 2019-2029,iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul
wakil kikwajuni Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaomba Washirika
Binafsi wa Sekta ya Viwanda pamoja na Wadau wa Maendeleo kuendelea
kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa Sera ya Viwanda Nchini ya
Mwaka 2019 – 2029 ili ifikie lengo la kuifanya Zanzibar kuwa ya
Viwanda.
Balozi
Seif alitoa ombi hilo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Vitabu
Vitano vya Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar iliyofanyika katika
Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Baloz Seif Ali Idi akitoa hotuba ya
Uzinduzi wa Sera ya Viwanda 2019-2029,iliofanyika katika Ukumbi wa
Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Alisema
Sera ya Viwanda ikiwa ni miongoni mwa Vitabu vilivyozinduliwa na kupata
baraka zote za Serikali itachangia kuimarika kwa Sekta hiyo kwa
kuzingatia utayarishaji wake imewashirikisha wadau wote wa Maendeleo ya
Viwanda na kuzingatia maoni na michango iliyotolewa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Sera hiyo ni matokeo ya mapitio ya
Sera ya Viwanda ya Mwaka 1998 iliyokuwa imepitwa na wakati ambayo pia
inakwenda sambamba na Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 – 2020 ibara ya 84
{d} inayozungumzia kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara.
Waziri
wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali akitoa Hotuba katika
hafla ya Uzinduzi wa Sera ya Viwanda 2019-2029,iliofanyika katika Ukumbi
wa Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Balozi
Seif alisema utekelezaji wa kazi zitaimarisha mazingira bora ya
Uwekezaji, uzalishaji wa bidhaa kupitia Viwanda vilivyopo ndani pamoja
na kuanzisha vipya ili Taifa lifanikiwe kukabiliana na tatizo la ajira
kwa Vijana, kuongeza mapato ya Serikali na kupunguza uagizaji bidhaa
kutoka nchi za nje.
“
Ninatambua kwamba kuitekeleza Sera ya Viwanda ni lazima kila Mshirika
apate fursa ya kusoma vitabu hivyo ili aweze kutimize wajibu wake
ipasavyo”. Alisisitiza Balozi Seif.
Muakilishi
kutoka Ubalozi wa Sweden Jenny Akeback akitoa hotuba katika hafla ya
Uzinduzi wa Sera ya Viwanda 2019-2029,iliofanyika katika Ukumbi wa
Sheikh Idriss Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba kwa vile Sera ya Viwanda
Zanzibar imeshapata baraka zote na kukubalika katika ngazi ya juu, hivyo
Serikali Kuu itajitahidi kuyatekeleza na kuyasimamia kwa upande wa
Sekta ya Umma.
Alielezea
kuwa vitabu vilivyozinduliwa vinategemewa kuwa na mwanzo mzuri wa
kukuza sekta ya Viwanda ambapo Wafanyabiashara watapata uelewa
kuhusiana na mazingira ya ufanyaji wa biashara pamoja na kupata
muongozo maalum utakaowasaidia wafanyabiashara na bidhaa kupitia daftari
maalum.
Muakilishi
kutoka UNIDO Steven Cargbo akitoa hotuba katika hafla ya Uzinduzi wa
Sera ya Viwanda 2019-2029,iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss
Abdul wakil kikwajuni Zanzibar.
Balozi
Seif aliwahakikishia Washirika wa Sekya ya Viwanda na Biashara kwamba
Serikali Kuu itazifanyia kazi changamoto zote zilizopo katika
urahisishaji biashara katika maeneo ya usafirishaji na uagizaji bidhaa,
usajili na uhaulishaji wa mali pamoja na upatikanaji wa vibali.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizitaka Mamlaka za utoaji wa leseni na
Mamlaka za usimamizi kuchukuwa hatua katika maeneo yote ambayo
hayakufanya vizuri ili kurahisisha ufanyaji biashara.
Katibu
Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Juma Hassa Reli akitoa hotuba ya
Makaribisho katika hafla ya uzinduzi wa Sera ya Viwanda
2019-2029-iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil
Kikwajuni Zanzibar.
Balozi
Seif alisema bado ipo kazi kubwa iliyo mbele kwa Taifa ya kuwaomba
Wawekezaji wengi zaidi kutumia fursa za Uwekezaji katika ujenzi wa
Viwanda Vipya huku akiwataka Wananchi waendeleze amani iliyopo
itakayowapatia ushawishi Wawekezaji hao.
Akitoa
salamu Mwakilishi kutoka Sekta Binafsi Bwana Ahmed Yussuf alisema Kundi
lao limepata faraja kubwa kutokana na ushiriki wao kwenye utayarishaji
wa Vitabu hivyo muhimu kwa Maendeleo ya Sekta ya Biashara Zanzibar.
Baadhi
ya waheshimiwa na Wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya
uzinduzi wa Sera ya Viwanda iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss
Abdull wakil kikwajuni Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Na Khadija Khamis -Maelezo Zanzibar.
Bwana
Ahmed alisema mchakato huo umeanza kwa muda kiasi, licha ya kuchelewa
lakini kilichozingatiwa ni umakini wa kusonga mbele na akashauri uwepo
wa ulinzi makini wa Viwanda vitakavyoanzishwa Nchini ili lile lengo
lililokusudiwa likamilike vyema.
Nao
kwa upande wao wakiwasilisha Salamu wa Taasisi zao, Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Viwanda {UNIDO} Bwana Stephen
na Mwakilishi wa Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania Bibi Jane Akebak
walisema mafanikio makubwa ya uimarishaji wa Sekta ya Viwanda
utafanikiwa vyema endapo Sera za Sekta hiyo zitaimarishwa na kuwa wazi.
Wameipongeza
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuliona hilo kwa uamuzi wake wa
kuandaa Sera, Miongozo na masuala mengine muhimu yanayojenga mazingira
bora ya kuendeleza Sekta ya Viwanda sambamba kwa kushirikisha Sekta
Binafsi.
Walieleza
kwamba Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Viwanda {UNIDO}
pamoja na Washirika wengine wataendelea kuiunga mkono Zanzibar katika
Mikakati yake ya kuvifanya Visiwa vya Zanzibar kuingia katika Mfumo wa
Viwanda katika uendeshaji wake wa Uchumi.
Walisema
Tafiti zitafanywa zinazokwenda sambamba na Wataalamu wa Taasisi hizo
kuendelea kutoa mafunzo kwa Vijana wa Zanzibar katika kuona Sekta ya
Viwanda inaendelea kusonga mbele kwa kipindi kirefu ikilenga kupunguza
tatizo la Ajira hasa kwa Vijana.
Walifahamisha
kwamba Sekta ya Viwanda Duniani imeanza tokea Karne ya 19 kwa kujikita
zaidi katika masuala ya Kilimo jambo ambalo wataalamu walipelekea
kubadilisha mfumo huo na kuelekeza nguvu zaidi katika furza zaidi za
ajira kwa kuanzisha uzalishaji wa biadhaa mbali mbali.
Akimkaribisha
mgeni rasmi kuzindua Vitabu hivyo Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi
Amina Salum Ali alisema uzinduzi wa Vitabu vya Sekta ya biashara umetoa
mwanga kwa safari ya Zanzibar kuelekea kwenye Maendeleo ya uhakika.
Balozi
Amina alisema Wizara ya Biashara itaendelea kubeba dhima ya kuiona
Zanzibar inastawi na kufanikiwa katika mwenendo mzima wa Sekta ya
Biashara inayotowa fursa kubwa katika utoaji wa ajira miongoni mwa
Wananchi walio wengi.
Wajasiri
amali wadogo wadogo wamezingatiwa katika mfumo wa Miongozo ya Sera na
Vitabu hivyo watakaokuwa na fursa pana zaidi ya kujengewa mazingira
mazuri wa bidhaa zao zitakazokuwa na muelekeo wa kuuzwa katika Masoko ya
Kimataifa likiwemo lile la AGOA.
Waziri
wa Biashara na Viwanda ameushiriki Uongozi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa unaoshughulika Viwanda {UNIDO} na Ubalozi wa Sweeden Nchini
Tanzania kwa michango yao iliyofanikisha kukamilika kwa Vitabu hivyo.
Jumla
ya Vitabu Vitano vimezinduliwa kuhusiana na Sera ya Viwanda, Ripoti ya
tathmini ya mazingira ya ufanyaji wa biashara, Daftari la
Wafanyabiashara, Muongozo wa usafirishaji na uagizaji pamoja na Taarifa
za Wazalishaji wa Kazi za Mikono Zanzibar zinazotarajiwa kuuzwa katika
Soko la AGOA.
No comments:
Post a Comment