Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa (kulia) akikagua jana chemba ya kutolea
upepo kwenye eneo la Uchama wilayani Nzega wakati alipopita kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani
Tabora.
Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa(katikati) akitoa maelekezo jana kwa
Mkandarasi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Tabora wakati
alipopita Wilayani Nzega kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo.
Meneja
Mradi kutoka WAPCOS Mattewada Manohar(mwenye T shirt )akimuonyesha
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa(kushoto) sehemu ya maungio ya
bomba la kupeleka maji Igunga na yale ya kwenda kwenye tenki la Ushirika
Nzega wakati alipopita Wilayani Nzega kukagua maendeleo ya ujenzi wa
Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani Tabora.
Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa (aliye mstari wa pili kushoto) akishuka
kutoka kwenye Tenki kubwa la maji lilipo Ushirika Wilayani Nzega wakati
alipopita jana kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa
Victoria kwenda Mkoani Tabora.STORY NA PICHA NA TIGANYA VINCENT
Serikali
inatarajia kutumia shilingi bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa
bomba za maji ya ziwa Victoria kutoka katika tenki la Ushirika lilipo
Nzega mjini kwenda Bukene .
Kauli
hiyo imetolewa jana na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati
alipopita Wilayani Nzega kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji
kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani Tabora.
Alisema
kuwa tayari fedha za ujenzi wa mradi huo zipo na usanifu wa mradi huo
umeshafanyika ambapo utakuwa umbali wa Kilometa 36 kutoka maji
yatakapochukuliwa kwenye tenki la maji la Ushirika lilipo Nzega mjini
hadi Bukene.
Profesa
Mbarawa alisema katika mpango wa awali Bukene haikuwepo kwenye mradi wa
maji kutoka Ziwa Victoria ,lakini Serikali imetafuta pesa kwa ajili ya
kujenga mradi huo.
Alisema
kwa kuwa fedha zipo kazi hiyo itaanza mara moja ambapo kukamilika
kwake utasaidia kutatua tatizo la maji katika Vijiji 19 vya Bukene kwa
kuwahakikishia wakazi wa eneo hilo wanapata maji safi na salama mapema.Aidha
Waziri huyo alisema utekelezaji wa mradi wa kuleta kutoka Ziwa Victoria
kwa ujumla umefikia asilimia 85 na anatarajia kuanzia mwezi Desemba
mwaka huu utakuwa umekamilika kwa kiwango kikubwa na wananchi wataanza
kupata maji safi na salama.
Aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inapeleka maji safi na salama kwa wananchi wengi ili kuwaondolea tatizo la maji.
Awali
Mhandisi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoani Tabora
(TUWASA), Athuman Kilundumya alisema zaidi ya watu 240,000 wanatarajia
kunufaika na ongezeko la eneo la utekelezaji wa mradi wa maji kutoka
ziwa Victoria katika Wilaya za Igunga, Nzega na Uyui.
Alitaja
maeneo ambayo yatanufaika kuwa ni Bukene wilayani Nzega ambapo Vijiji
19 vitapata maji hayo, Nkinga wilayani Igunga vijiji saba na Kigwa
wilayani Uyui , vijiji 16 vya Kata za Igalula, Goweko na Kigwa navyo
vinatarajia kupata maji hayo.
Kiludumya
alisema kuwa utekelezaji wa mradi wa kuleta maji toka Ziwa Victoria
huko katika hatua nzuri na ndani ya wiki tatu maji yatakuwa yamefika
katika Manispaa ya Tabora.
No comments:
Post a Comment