Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa
Takukuru Mkoa maalumu wa Kinondoni kumchunguza Mkandarasi wa Savei anayesimamia
urasimishaji makazi ya wananchi kanda ya Madale two , David Emanuel kutokana na
tuhuma ya kudaiwa kuiba kiasi cha shilingi milioni 52 fedha zilizochangwa na
wananchi.
Ameongeza kuwa milioni 52 zimelipwa pasipokufuata utaratibu kutokana na
mkandarasi huyo kuwa sehemu ya waweka saini katika akaunti ya wananchi na kwamba
alichokuwa anakifanya nikwenda mwenyewe benki na kuchukua fedha.
Mhe. Chongolo amefikia uamuzi huo katika kikao chake na
Kamati zilizoundwa na wananchi kwa ajili ya kuratibu na kusimamia zoezi la
urasimishaji pamoja na wakandarasi waliopewa jukumu la urasimishaji makazi ya
wananchi katika Halmashauri hiyo.
Mhe. Chongolo ameeleza kuwa mkandarasi huyo alijilipa mwenyewe fedha
hizo pasipokufuata utaratibu na kwamba kitendo hicho ni matumizi mabaya
ya fedha za wananchi na kuagiza Takukuru Kinondoni kumchukulia hatua
pindi atakapobainika ukweli dhidi ya tuhuma hizo.
Amefafanua kuwa katika kanda hiyo, viwanja zaidi ya 1800 vimerasimishwa
na hivyo wananchi wamechanga kiasi cha shilingi zaidi ya milioni 70 na kwamba
hadi sasa mkandarasi huyo ameshalipwa shilingi milioni 62 ambapo kati ya hizo
milioni 12 ndio zilizolipwa kwa kufuata utaratibu.
“ Sasa ukiona hivi unajua kabisa kunachangamoto ya matumizi yasio
yasihi ya fedha za wananchi,nimechukua hatua nimemkabidhi Kamanda wa Takukuru
mkoa maalumu wa Kinondoni, wamemchukua wanakwenda kushugulikia kufanya
uchunguzi na pale watakapobaini kunaukiukwaji watamchukulia hatua” amesema Mhe.
Chongolo.
Nakuongeza kuwa” kulingana na changamoto ambayo tumeibaini leo kwenye
mtaa mmoja, nimeagiza kitengo cha ukaguzi wa ndani kwenda kukagua akaunti zote
za urasimishaji ndani ya Halmashauri yetu ,ili kujiridhisha na yale watakayo
yabaini sisi watuletee ripoti ilituweze kuchukua hatua stahiki kwa wakati
muafaka”.
Awali Mhe. Chongolo amesema kuwa katika mkutano huo wanapokea taarifa ya
kila mkandarasi juu ya mwenendo na matumizi ya fedha zinazochangwa kutoka kwa
wananchi ilikukamilisha zoezi husika la urasimishaji.
Amebainisha kuwa , katika mkutano huo amejifunza kuwepo na changamoto ya
usimamizi wafedha za wananchi katika maeneo mengi yanayoendesha zoezi hilo ipo
haja ya haraka katika kutatua changamoto hizo.
No comments:
Post a Comment