Mabadiliko
ya Mfumo wa Utendaji Kazi wa shirika kutoka Kiraia kuwa Jeshi-Usu
Chini ya uongozi wa awamu ya tano, TANAPA imeweza kufanya
mabadiliko makubwa katika eneo la mfumo wa utendaji kazi kutoka ule wa Kiraia
kwenda Jeshi-Usu. Muundo mpya wa Shirika uliidhinishwa na Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na kuzinduliwa
rasmi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Novemba, 2018. Hadi kufikia
leo jumla ya watumishi 1,919 ambao ni asilimia 86 ya watumishi 2,230 ambao ni
kuanzia ngazi ya Kamishna wa Uhifadhi hadi Askari wa Uhifadhi wa kada
mbalimbali, wamepatiwa mafunzo ya mabadiliko ya mfumo.
Ongezeko
la Hifadhi mpya za Taifa
Tangu
kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa mwaka 1959 hadi mwezi Oktoba 2016,
Shirika lilikuwa likisimamia hifadhi 16 nchini. Katika kipindi cha Miaka Minne
ya Awamu ya Tano, Hifadhi za Taifa nyingine sita (3) za Burigi – Chato; Ibanda – Kyerwa; Rumanyika – Karagwe. Aidha,
hatua mbali mbali zinaendelea za kuyafanya yaliyokuwa Mapori ya Akiba ya Selous
kupandishwa hadhi na kuongeza hifadhi nyingine mpya za Nyerere; Kigosi na Mto
Ugala ambapo kukamilika kwa hatua hizi kutafanya jumla ya Hifadhi za Taifa
kufikia 22 ambazo kwa ujumla wake zitakuwa na eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 104,559.1 ambalo ni takribani asilimia 11 ya
eneo la nchi yetu ya Tanzania.
Aidha, TANAPA imeshaanza utekelezaji wa usimamizi wa
majukumu katika hifadhi hizi mpya ambayo inalenga kupanua wigo wa utalii wa
ukanda wa Kaskazini Magharibi ambao utaunganisha hifadhi hizi na Hifadhi za
Kisiwa cha Rubondo, Kisiwa cha Saanane na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Ongezeko la Mapato
Katika kipindi cha Awamu ya Tano, TANAPA imeweza
kuongeza mapato ikilinganishwa na makadirio yaliyokuwa yakiwekwa kila mwaka. Shirika
limeweza kuongeza mapato kutoka kiasi cha shilingi 175,089,696,000 kilichokusanywa
mwaka wa fedha 2015/16; shilingi 207,587,218,000
zilikusanywa mwaka 2016/17 na shilingi 254,794,242,000 mwaka 2017/18 hadi
kufikia kiasi cha shilingi 279,406,200,806 mwaka wa fedha 2018/2019 ikiwa ni
ongezeko la shilingi 566,697,964,806 kwa miaka mitatu sawa na asilimia 60.
Ongezeko la mapato
ya shirika limetokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa ndani na nje ya nchi
ili kuyafikia masoko mapya ambapo liliwezesha kuwa na ongezeko la watalii kutoka wageni 957,576 mwaka 2015/16 hadi 1,141,462
mwaka 2018/19 ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.2
Mchango wa Kodi
Serikalini
TANAPA imeongeza mchango wa
kodi kwa serikali kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2016/2017 hadi kufikia
shilingi bilioni 42 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Katika kipindi hiki cha miaka minne ya uongozi wa
awamu ya tano, TANAPA imeweza kutenga fedha kiasi cha shilingi
111,374,526,023.00 ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika
kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 hadi 2018/2019. Miradi hii imehusisha
uimarishaji wa huduma za utalii ikiwemo ujenzi wa maeneo ya malazi ya gharama
nafuu (mabanda na hosteli), miradi ya kuongeza bidhaa za utalii, nyumba za
wafanyakazi, vifaa vya kazi kama boti, magari na ndege.
Utatuzi wa Migogoro ya Mipaka na Wananchi
Shirika la Hifadhi za Taifa limeweza kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini baina ya hifadhi na wananchi wanaozunguka hifadhi.
Mwaka
2018/2019 Shirika kupitia Mpango wake wa Ujirani Mwema unaoshirikisha jamii
katika uhifadhi, liliamua kushirikiana na vijiji vilivyo pembezoni mwa Hifadhi
za Taifa kuandaa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi pamoja na kuweka alama za
kudumu za mipaka kwenye mipaka yote ya Hifadhi.
Kuandaa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kumekuwa na jitihada kubwa za kukabiliana na
changamoto za migogoro ya ardhi ikiwemo mipaka na uingizaji mifugo kwa ajili ya
malisho. Kutokana na jitihada hizo, Shirika linagharamia kazi ya kuandaa na kuwezesha mipango ya
Matumizi Bora ya Ardhi ya vijiji vinavyozunguka Hifadhi za Taifa Tanzania kwa
kutumia utaalamu wa tume ya Taifa
ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ‘National Land Use Planning Commission - NLUPC’
yenye
mamlaka kisheria. Lengo kuu likiwa ni kuviwezesha vijiji 392 vilivyokuwa
vimeainishwa kutokuwa kuwa na mipango hiyo. Hata idadi hii itaongezeka kwa sababu
ya Hifadhi mpya ambazo zimeanzishwa. Awamu ya Kwanza ya utekelezaji wa kazi hii
ilianza mwaka wa fedha 2018/2019 kwa kuvilenga vijiji 95 ambavyo kutokana na
baadhi ya vitongoji kuwa vijiji, idadi iliongezeka kufikia vijiji 107
vinavyopakana na Hifadhi za Taifa za Serengeti, Ziwa Manyara na Tarangire.
Aidha, kwa kipindi
hiki cha miaka minne Serikali kupitia Shirika la TANAPA imetekeleza miradi
katika vijiji 101 vinavyopaka Hifadhi za Taifa ikiwemo ujenzi wa vyumba vya
madarasa (76), nyumba za walimu (19), mabweni (7), visima vya maji (10),
maabara (5), zahanati (10), mabwalo ya chakula (4), lambo la maji (1), madawati
(2,175), majengo ya utawala / ofisi ya walimu (10), nyumba za waganga (16),
mizinga ya nyuki (1,497), nyumba kwa ajili ya kuzalisha uyoga (1), miradi ya
ufugaji wa samaki (2), kuanzisha Benki za Uhifadhi za kijamii (21), kutoa taa
za umeme-jua kwa ajili ya vikundi vya uvuvi (80), boti kwa ajili ya vikundi vya
uvuvi (2), Injini za boti kwa ajili ya vikundi vya uvuvi (2).
Vita Dhidi ya Ujangili
na Ongezeko la Idadi ya Wanyama walio hatarini kutoweka
TANAPA imeweza kuimarisha mifumo ya ulinzi wa
wanyamapori na ustawi wa wanyama adimu na kupelekea ongezeko la wanyama adimu jamii ya
faru kwa asilimia 10 katika Hifadhi za Taifa na kudhibiti vitendo vya ujangili
kwa zaidi ya asilimia 90. Aidha Majangili 14,464 wamekamatwa na kufikishwa
katika vyombo mbalimbali ya dola nchini.
Ongezeko la
Masoko Mapya ya Watalii na idadi ya vitanda
Kumekuwepo
na ongezeko la idadi ya watalii wa nje kutoka 518,457 hadi 715,314 kutokana na kuongezeka kwa wigo wa soko la utalii katika masoko mapya
katika Bara la Asia na Mashariki ya Mbali hususani Israeli, Uturuki, China na
Urusi.
Aidha, kumekuwepo
na ongezeko la vitanda
vya watalii kutoka vitanda 2400 hadi kufikia vitanda 5,829 vya watalii wa nje
(international tourists), na vitanda 3,601 hadi kufikia 4,970 vya wageni wa
ndani (domestic tourists) na kufanya jumla ya vitanda vyote kufikia 10,799
Utekezaji wa Miradi mbalimbali ya Kimkakati kama vile:
i.
Ununuzi
wa kivuko katika Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo
ii.
Ujenzi
wa hoteli ya hadhi ya nyota tatu katika Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo
iii.
Ujenzi
wa uwanja wa mpira wa golfu katika Hifadhi ya Taifa Serengeti
iv.
Ununuzi
wa boti ya kifahari ya kitalii katika hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane
v.
Ujenzi
wa eneo maalumu la kuhifadhi wanyama aina ya faru kwa ajili ya shughuli za
kitalii katika Hifadhi ya Taifa Mkomazi.
Kuongezeka kwa huduma za utalii kama vile:
i.
Utalii
wa Puto (Baloon safaris)
ii.
Uendeshaji
wa farasi (Horse riding)
iii.
Upandaji
Mlima Kilimanjaro kwa kutumia baiskeli (mountain cycling)
iv.
Kuruka
na mwavuli (paragliding)
v.
Kuhamisha
na kupandikiza wanyama katika hifadhi mbalimbali
No comments:
Post a Comment