Picha ya pamoja Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema
leo, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse ,Ikulu
jijini Dodoma.
Bw.
Tadesse akiwa ameambatana na ujumbe wake amewasili uwanja wa ndege wa
jijini Dodoma leo, Novemba 25, 2019 na kulakiwa na Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, na Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A.
Ibuge.
Akizungumza
muda mfupi baada kumaliza mazungumzo na Mheshimiwa Rais Magufuli, Bw.
Tadesse amesema TDB itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya
Tanzania na kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya
kutekeleza miradi mbalimbali maendeleo nchini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB)
Bw. Admassu Tadesse wakifurahia jambo mara baada ya mazungumzo
yaliyofanyika Ikulu jijini Dodoma
Mhe.
Dkt. Mpango amesema TDB imekuwa moja ya Benki kinara ambayo imekuwa
ikitoa mikopo ya masharti nafuu kwa Tanzania hivyo kuchangia kwa kiasi
kikubwa kwenye miradi ya maendeleo.
Aidha,
Bw. Tadesse akiwa nchini atatembelea maeneo mbalimbali sambamba na
kujionea miradi ya maendeleo inayotelezwa na Serikali ikiwemo miradi ya
ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji, mradi wa kuzalisha umeme wa Kilwa
na miradi mingine ambayo mkopo kutoka (TDB) utaelekezwa.
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB)
Bw. Admassu Tadesse akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa ndege wa jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati), Mkuu wa Itifaki
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Kanali Wilbert A. Ibuge (mweji vazi la Jeshi) na Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Mipango Bw. Doto James (Watatu kushoto) wakijongea usawa wa
ndege kumlaki Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini
mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse alipowasili jijini Dodoma Novemba
25, 2019.
Mkuu
wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akisalimiana na Rais wa Benki
ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw.
Admassu Tadesse wakati anawasili jijini Dodoma.
Viongozi
na Watendaji wa Serikali wakiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse mara
baada ya kumlaki katika uwanja wa ndege jijini Dodoma.
chanzo Michuziblog
No comments:
Post a Comment