Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amemuelekeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. Selemani Jafo kufanya mabadiliko kwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara na
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, zilizopo katika Mkoa wa Morogoro kama
ifuatavyo;
1.
Halmashauri ya Mji wa Ifakara iongezwe
idadi ya Kata, kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Makao
Makuu yawe Ifakara Mjini.
2.
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ibadilishwe
jina, na iitwe Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba.
Makao
Makuu yawe Mgeta kama ilivyoamuliwa na Baraza la Madiwani.
Mhe. Rais Magufuli amewasisitiza
viongozi wa halmashauri kutowayumbisha wananchi na watumishi kuhusu utekelezaji
wa maelekezo hayo.
Mhe. Rais Magufuli
amemuagiza Mhe. Waziri Jafo kusimamia utekelezaji wa maelekezo hayo kwa mujibu
wa sheria
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Novemba,
2019
No comments:
Post a Comment