Moja ya bomba la Maji likiwa linatoa Maji mengi wakati Wa kusafisha mabomba.
Serikali
imesema kuwa imeridhishwa na utekelezaji Wa mradi mkubwa Wa Maji Wa
shilingi bilioni 520 unaotekelezwa katika halmashauri ya jiji la Arusha
utakao hudumia wananchi .
Akizungumza
na Waandishi Wahabari Mara baada ya kukagua miundombinu ya mradi huo
,Mkurugenzi Wa Idara ya usambazaji Wa Maji na Usafi Wa mazingira kutoka
Wizara ya Maji ,Nadhifa Kemikimba alisema kuwa amerithishwa na kasi ya
ujenzi Wa mradi huo huku akibainisha kuwa nia ya serikali nikuona hadi
ifikapo mwaka 2020 upatikanaji Wa huduma za Maji kwa Mjini umefikia
asilimia 95% huku vijijini wananchi wanapata Maji kwa asilimia 85%.
mkuu
wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa maelekezo kwa mkandarasi mara
baada ya kutembelea moja ya kisima cha maji ya mradi wa shilingi bilioni
520 kilichopo Ngaramtoni ndani ya wilaya ya Arumeru ambapo alimtaka
mkandarasi kuhakikisha adi ifikapo November 30 wananchi wawe wameanza
kupata maji
Kwa
upande wake kaimu mkurugenzi AUWSA Mhandisi Justine Mwangijomba alisema
kuwa mradi huo umefikia hatua ya kusafisha mtandao Wa mabomba
yanayopeleka Maji kwenye tanki pamoja na kuweka Maji dawa tayari kabisa
kwa ajili ya wananchi kuanza kutumia.
"Kama
ulivyoona tumepita katika matanki yetu ya Maji natumeona tanki moja la
Lita milioni kumi tumeanza kuweka Maji kwani ujenzi Wa tanki hilo
umekamilika hivyo muda sio mrefu wananchi watapata ongezeko la Maji na
tutaanza kuwapa wale wenye matatizo ya Maji kama muriet na olasiti"
alisema Mwangijomba.
Kaimu
mkurugenzi wa mamlaka ya maji AUWSA Mhandisi Justine Mwangijomba akimpa
maelekezo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo jinsi maji yanavyoingia
katika tanki kubwa la lita milioni 10 ambalo limekamilika na jana
november 24 zoezi la usafishaji mabomba kwa ajili ya matumizi ya
binadamu ,tanki hilo kubwa lipo mji mdogo wa ngaramtoni ndani ya wilaya
ya Arumeru maji haya ni ya mradi wa kiasi cha shilingi bilioni 520
uliotolewa na serikali na yatahidumia jiji zima la Arusha (picha na
Woinde Shizza,Arusha).
Mkurugenzi
Wa Idara ya usambazaji Wa Maji na Usafi Wa mazingira kutoka Wizara ya
Maji ,Nadhifa Kemikimba akiongea na wakandarasi na wafanyakazi Wa AUWSA
Mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kutembelea mradi mkubwa Wa
shilingi bilioni 520.(picha na Woinde Shizza Arusha) .
Akiongelea
mradi huo Mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa kuna ujenzi
Wa makao makuu ya mamlaka ya Maji safi na Maji taka ambao ulikuwa
unasuasua lakini baada ya OFISI yake kwakushirikiana na msimamizi Wa
mkandarasi kufatilia kwa makini ujenzi huo umeanza kwenda vizuri
Akibainisha
kuwa walipotembelea mradi huo ujenzi ulivyokuwa ukisuasua ulikuwa
umefikia asilimia 7.5 lakini baada ya kuusimamia vizuri umeongezeka na
kufikia asilimia 10 ambapo alibainisha mbali nakufuatilia mradi huo pia
wamempa mkandarasi mashariti ya kufanya Kazi usiku na mchana
,kuwasilisha taarifa za mradi unavyoendelea kila wiki huku akimtaka
ajenge kwa kufuata vipimo vinavyotakiwa na katika ubora unaotakiwa
Kwa
upande wake Mkuu Wa wilaya ya Arusha alisema kwamba kumalizika kwa mradi
huo kutawasaidia wakazi Wa jiji la Arusha kuondokana na tatizo la Maji .Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
No comments:
Post a Comment