Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenerali, Venance Mabeyo (kushoto), Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi, Simon Siro (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa, Diwani Athumani (kulia) baada ya wote kushiriki katika
mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika
katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akishirika katika sala ya kumwombea marehemu kaka
yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika katika kijiji cha Nandagala
wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la kaka yake, Mzee
Bakari Majaliwa katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nandagala
wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika sala ya kumwombea marehemu
kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika nyumbani kwa marehemu
katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewashukuru watu wote waliojitokeza katika
mazishi ya kaka yake Mzee Bakari Majaliwa (78), aliyefariki juzi
(Jumatatu, Novemba 04, 2019) nyumbani kwake katika kijiji cha Chimbila
‘B’wilayani Ruangwa, Lindi.
Ametoa
shukrani hizo leo (Jumatano, Novemba 06, 2019) wakati wa ibada ya
mazishi iliyofanyika kijijini Nandagala wilayani Ruangwa na amesema
kwamba hayo ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kila mtu atapita kwenye njia
hiyo.
“Tulikuwa
12 na sasa tumebaki watano, wanaume wawili na wanawake watatu. Msiba
huu kwetu ni mkubwa umepunguza idadi ya watoto wa Mzee Majaliwa lakini
hatuna namna ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu, wajibu wetu ni kuendelea
kumuombea. Nawashukuru wote mlioacha shughuli zenu na kutukimbilia,
familia imethamini sana ujio wenu jambao hili limetokea ghafla.”
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi, Simon Siro katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari
Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa,
Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa, Diwani Athumani katika mazishi ya kaka yake Waziri
Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala
wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenerali Venance Mabeyo katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee
Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani
Ruangwa, Novemba 6, 2019. Wa pili kulia ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi, Simon Siro.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu pia amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa salamu za pole
alizozitoa. “Jambo hili pia limemgusa Mheshimiwa Rais wetu ambaye
ametutaka tuwe watulivu katika kipindi hiki kigumu na kwamba kila mmoja
kwa dhehebu lake aendelee kumuombea marehemu ili Mwenyezi Mungu amlaze
mahala pema.”
Kwa
upande wake, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Generali, Venance
Mabeyo akitoa salamu za pole kwa niaba ya Maafisa na Askari wa Vyombo
vyote vya Ulinzi na Usalama amesema anajua uzito wa msiba pamoja na
majonzi waliyonayo kwa kuondokewa na mpendwa wao na kwamba wamshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kuwa ndiye anayetoa na anayetwaa. “Hakuna namna ya
kurekebisha maamuzi ya Mwenyezi Mungu, tuendelee kumsindikiza kaka yetu
kwa sala Mwenyezi Mungu ampokee kwa amani.”
Naye,
Mwakilishi wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Othman Kaporo
amesema amewataka wananchi wajiandae na kifo kwa kufanya ibada. “Ni
kawaida kwa binadamu kujisahau lakini Mwenyezi Mungu ametuwekea vitu vya
kutukumbusha juu ya uwepo wake ikiwemo kifo, hivyo tuyatekeleze yale
yalikuwa ya wajibu kuyatekeleza.”
No comments:
Post a Comment