Thursday, January 30, 2020
TANZANIA HAINA MGONJWA WA CORONA - WAZIRI UMMY
Mpaka sasa Tanzania haina Mgonjwa wala muhisiwa wa ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha Coromna (Hona kali ya mafua) hata hivyo kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo hasa kibiashara na kijamii kati ya Tanzania na nchi za bara la Asia ikiwemo nchi ya China nchi inakuwa katika hatari pia ya ugonjwa huo.
Haya yamesemwa na Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa tarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugponjwa huo jijini hapa.
Haya yamesemwa na Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa tarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugponjwa huo jijini hapa.
Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu |
“Ugonjwa huu unasababiswa na kirusi jamii ya Corona na ni kipya “Novel (New) Corona virus 2019” (2019-nCOV) ambacho ni tofauti na virusi vingine vya jamii hiyo ambavyo viliwahi kusababisha milipuko ya ugonjwa uliojulikana kama ‘SARS-CoV’ mwaka 2003 na MERS-CoV Corona Virus mwaka 2013”.Amesema Waziri Ummy.
Aidha, waziri Ummy amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya hewa kwa kuingiwa na majimaji yenye virusi kutoka mtu mmoja kwa njia ya kukohoa au kupiga chafya au kwa kugusa majimaji au makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na dalili za ugonjwa huo na dalili huanza kuonekana kati ya siku moja hadi kumi na nne tangu kupata maambukizo.
Hata hivyo ametaja dalili za ugonjwa huu ni pamoja na Homa, mafua, kuumwa kichwa, mwili kuchoka, kikohozi, kubanwa mbavu, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, mapafu kuathirika, kupumua kwa shida na hata kifo.
“Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja, hivyo kama yalivyo magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi, matibabu hufanyika kwa kuzingatia dalili zilizopo na ufuatiliaji wa karibu” Amesisitiza Waziri Ummy.
Wakati huo huo waziri huyo amewashauri wananchi kuchukua hatua ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuzingatia kanuni za afya na usafi ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na mtu mwenye dalili za mafua mwenye historia ya kusafiri katika nchi zilizokumbwa na mlipuko na kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kitambaa safi au nguo uliyovaa sehemu za mikono
“Kutokana na mwenendo na kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huo kipindi hiki cha mlipuko, Wizara inashauri kusubiri na kuepuka safari zisizo za lazima kwenda kwenye maeneo yaliyoathirika na inapolazimu kusafiri basi
Monday, January 27, 2020
SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU VIRUS VYA CORONA NCHINI CHINA
Serikali imewataka watanzania kuwa watulivu,makini na
kupenda kuwa na subira ya kupata maelezo,maelekezo na ufafanuzi rasmi wa
Serikali pale kunakotokea jambo badala ya kukimbilia kwenye mitandao na uvumi
ili kuondoa kueneza hali ya taharuki kwa wananchi bila ya kuwa na uhakika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya
hali ya Watanzania waishio nchini China kutokana na kuzuka kwa virusi vya homa
ya corona nchini humo.
Prof. Kabudi amesema Tanzania ina wanafunzi takribani 4000
ambapo katika mji wa Wuhan kuna wanafunzi 400 na kwamba kwa mujibu wa Balozi wa
Tanzania Nchini China Balozi Mbelwa Kairuki ameihakikishia serikali kuwa mpaka
sasa hakuna mtanzania yeyote aliyeathiriwa ama kukumbwa na maradhi hayo.
Ameongeza kuwa Tanzania inaendelea kufuatilia kwa ukaribu
kujua maendeleo na hali za watanzania wanaoishi jimboni Wuhan na China kwa
Ujumla.
Aidha amewataka Watanzania kuwa makini na suala la kutoa
taarifa zisizo rasmi ama uvumu kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za
Tanzania na kuwataka kuwa na Subira kupata taarifa rasmi kutoka serikalini.
NENDENI MKACHAPE KAZI KWA UADILIFU NA KUTANGULIZA MASLAHI YA TANZANIA - RAIS MAGUFULI
Viongozi waliopishwa wakila kiapo cha Uadilifu kwa vioungozi wa Umma Ikulu jijini Dar es Salaam |
- Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 27 Januari, 2020 amewaapisha Mawaziri 2 na Mabalozi 3 aliowateua hivi Karibuni.
- Mawaziri walioapishwa ni George Boniface Mwataguluvala Simbachawene aliyeapishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mussa Azzan Zungu aliyeapishwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam. |
- Mabalozi walioapishwa ni Mhe. Maimuna Kibenga Tarishi aliyeapishwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva – Uswisi, Hussein Athuman Kattanga aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Tokyo – Japan na Prof. Kennedy Godfrey Gastorn aliyeapishwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa New York Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mussa Azzan Zungu kuwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. |
- Akizungumza baada ya kuwaapisha na kushuhudia wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, Rais Magufuli amewataka viongozi hao kwenda kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uchapakazi, kutanguliza maslahi ya Tanzania pamoja na kushirikiana vizuri na viongozi na watendaji wengine katika wizara zao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Hussein Kattanga kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan |
- Amemtaka Mhe. Waziri Simbachawene kushughulikia dosari zilizopo katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwemo kuhakikisha watendaji na viongozi ambao ni kikwazo katika ufanisi wa wizara wanaondolewa, pamoja na kushughulikia makubaliano yaliyotiwa saini na viongozi wakuu wa wizara waliopita kuhusu mkataba wa ununuzi wa vifaa vya zimamoto (vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni 1) katika mazingira yasiyokuwa na uadilifu na bila kujali maslahi ya Taifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Kennedy Gastorn kuwa Balozi wa kudumu wa Tanzania, Umoja wa Mataifa New York katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. |
- Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na imehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene Nyaraka zenye makubaliano (MoU) zilizotiwa saini na Viongozi wakuu wa Wizara hiyo ambao hawapo kwasasa kuhusu ununuzi wa vifaa mbalimbali vya Jeshi la Zimamoto ili aifanyie kazi haraka. |
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu akizungumza mara baada ya kuapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Maimuna Tarishi kuwa Balozi wa kudumu wa Tanzania umoja wa Mataifa Geneva |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene akila kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. |
Sunday, January 26, 2020
KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI YATEMBELEA KIWANDA CHA ALAF
Wajumbne wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mitaji ya Umma, wakiangalia jinsi uzalishaji unavyofanyika katika Kiwanda cha ALAF jijini Dar es Salaam walipotembelea ijumaa.
Kamati
ya Bunge ya Uwekezaji ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Raphael
Chegeni, leo imefanya ziara katika kiwanda cha ALAF jijini Dar es
salaam.
Madhumuni ya ziara hii ni kuipa Kamati hiyo uelewa zaidi kuhusu shughuli mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa zinazofanywa na kiwanda hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Kiwanda cha ALAF, Wilberforce Msokwa akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bune ya Kudumu ya Mitaji ya Umma walipotembelea kiwanda hicho.
Tarehe
14 Januari mwaka huu, Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Dipti Mohanty
alipata mwaliko wa kuhudhuria kikao cha Kamati hiyo ya Bunge ya
Uwekezaji, ambapo alipata fursa ya kuelezea mafanikio ya kampuni hiyo na
changamoto mbalimbali za kibiashara.
Kamati hiyo iliipongeza ALAF kwa mafanikio makubwa iliyopata hivi karibuni, na kuahidi kuitembelea kampuni hiyo, ahadi ambayo imetimizwa leo na Mwenyekiti wa Kamati pamoja na Wajumbe wote.
Kamati hiyo iliipongeza ALAF kwa mafanikio makubwa iliyopata hivi karibuni, na kuahidi kuitembelea kampuni hiyo, ahadi ambayo imetimizwa leo na Mwenyekiti wa Kamati pamoja na Wajumbe wote.
Meneja wa Usalama pakazi wa Kiwanda cha ALAF, Fredrick Nowi (katikati) akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kuduma, Dk Raphael Chegeni (kushoto) wakati wajumbne wa kamati hiyo walipotembelea kiwanda hicho.
Katika ziara hiyo, Kamati
imepata fursa ya kutembelea kiwanda cha ALAF na kujionea hatua za
uzalishaji, bidhaa na huduma mbalimbali. Pamoja na kukutana na baadhi ya
wafanyakazi wa ALAF, pia walitembelea kituo cha afya kinachotoa huduma
za matibabu kwa wafanyakazi na familia zao,.
Mtendaji Mkuu, Dipti Mohanty ameishukuru Kamati ya Bunge ya Uwekezaji kwa kupata muda wa kutembelea ALAF. Mtendaji Mkuu huyo ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi zake za kujenga Tanzania ya viwanda, na kuikaribisha Kamati hiyo kutembelea ALAF tena.
Fundi Mitambo na Uzalishaji wa Kiwanda cha ALAF, Paul Luambano (kulia) akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mitaji ya Umma jinsi mitambo inavyofanya kazi wakati kamati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea kiwandani hapo kuangalia jinsi uzalishaji unavyofanyika
Mtendaji Mkuu, Dipti Mohanty ameishukuru Kamati ya Bunge ya Uwekezaji kwa kupata muda wa kutembelea ALAF. Mtendaji Mkuu huyo ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi zake za kujenga Tanzania ya viwanda, na kuikaribisha Kamati hiyo kutembelea ALAF tena.
Fundi Mitambo na Uzalishaji wa Kiwanda cha ALAF, Paul Luambano (kulia) akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mitaji ya Umma jinsi mitambo inavyofanya kazi wakati kamati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea kiwandani hapo kuangalia jinsi uzalishaji unavyofanyika
Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji, Mhe. Raphael Chegeni, alisema wamekuja
kuangalia jinsi gani wanaweza kusaidia ukuwaji wa sekta ya viwanda
pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo upatikanaji wa nishati
ya umeme wa hakika pamoja na malipo ya VAT zinazodaiwa kutoka kwa
mamalaka ya mapato TRA.
TANZANIA, INDIA ZAAHIDI KUENDELEZA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA, KUKUZA MAENDELEO
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.
Damas Ndumbaro (Mb) akiwasilisha hotuba yake wakati wa maadhimisho ya
miaka 71 ya Jamhuri ya India yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika
ofisi za Ubalozi wa India jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Balozi wa
India nchini Tanzania, Dan Kohli
Tanzania
na India zimeahidi kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia pamoja na
kushirikiana katika kuhakikisha kuwa na maendeleo endelevu baina ya nchi
hizo mbili.
Akihutubia sherehe za maadhimisho ya 71 ya Jamhuri ya India, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kuwa Tanzania na India ni ndugu na nchi hizo zitaendelea kushikiana katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya diplomasia ya uchumi baina ya nchi hizo yanakuwa kila wakati.
Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Balozi Shri Sanjiv Kohli akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 71 ya Jamhuri ya India yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Ubalozi wa India jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro.
Akihutubia sherehe za maadhimisho ya 71 ya Jamhuri ya India, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kuwa Tanzania na India ni ndugu na nchi hizo zitaendelea kushikiana katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya diplomasia ya uchumi baina ya nchi hizo yanakuwa kila wakati.
Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Balozi Shri Sanjiv Kohli akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 71 ya Jamhuri ya India yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Ubalozi wa India jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro.
“Nchi ya Tanzania na India zina uhusiano mzuri, imara na
wa muda mrefu ulianzishwa na baba wa Taifa Mwl. Julias Nyerere pamoja
na Mahatma Gandhi. Na uhusiano huu umekuwa ukisaidia kuimarisha
maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa” alisema Dkt. Ndumbaro
Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa “sisi Tanzania na India ni ndugu, kwa hiyo basi tunawatakia sana kila la kheri katika kuiletea India maendeleo…lakini pia tukumbuke kuwa maendeleo ya India ni maendeleo ya Tanzania pia,”
Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa “sisi Tanzania na India ni ndugu, kwa hiyo basi tunawatakia sana kila la kheri katika kuiletea India maendeleo…lakini pia tukumbuke kuwa maendeleo ya India ni maendeleo ya Tanzania pia,”
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia/kusikiliza hotuba ya mgeni rasmi
(Dkt. Ndumbaro) hayupo pichani wakati wa sherehe za maadhimisho ya
miaka 71 ya Jamhuri ya India yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika
ofisi za Ubalozi wa India
Kwa sasa uchumi wa India na Tanzania umezidi kukuwa na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya mataifa hayo. India imekuwa msharika mzuri wa maendeleo nchini Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo utalii, maji, afya, teknolojia na elimu. Msaada wa India katika sekta ya maji hadi sasa, imeweza kusaidia kusambaza maji safi na salama katika kwa jiji la Dar es Salaam pamoja na upanuzi na uboreshaji wa mitambo ya maji Zanzibar.
Aidha, kwa upande wa sekta ya elimu, Tanzania na India zimeshasaini makubaliano ya kushirikiana kujenga kituo cha ufundi na pia msaada wa kuendeleza vyuo vikuu vya Zanzibar ambavyo vinatoa ujuzi unaolengwa kuwaendeleza wanawake walio na elimu ndogo au isiyo rasmi.
Kwa upande wake, Balozi wa India chini Tanzania, Mhe. Balozi Shri Sanjiv Kohli ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa umoja na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa India na kusema kuwa umoja huo umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa Tanzania na Taifa la India.
“Napenda kuwafahamisha kuwa umoja na mshikamano wetu umekuwa chachu ya maendeleo baina ya mataifa haya mawili…..tukumbuke kuwa umoja ni nguvu na dhamira yetu ni kushirikiana na mataifa yote duniani. Na dhamira yetu ni kuishi kwa amani umoja na mshikamano ili kukuza uchumi wetu,” Alisema Balozi Kohli
Aidha, Balozi Kohli amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuwa ya kipekee kwa taifa la India kutokana na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa nchi ya India kijamii, kisiasa na kiuchumi.
“India inajivunia kuwa na uhusiano na mzuri na Tanzania ambao umewezesha mataifa haya kufanya biashara, uwekezaji, kujenga uwezo, ujenzi wa miundiombinu pamoja na maendeleo ya kiuchumi,” ameongeza Balozi Kohli.
WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGA SEMINA YA VIONGOZI WA DOLA KUHUSU USIMAMIZI NA UDHIBITI WA MADINI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza wakati alipofunga semina ya Viongozi wa Dola katika
Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali Madini kwenye ukumbi wa St. Gaspar
jijini Dodoma, Januari 26, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiagana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi baada
ya kufunga semina ya Viongozi wa Dola katika Usimamizi na Udhibiti wa
Rasilimali Madini kwenye ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma, Januari 26,
2019. Kulia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko , Wa tatu kulia ni Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini, Stanslaus Nyongo na wapili kushoto ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila
Baadhi ya washiriki wa semina ya
Viongozi wa Dola katika Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali Madini
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofunga semina hiyo
kwenye ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma, Januari 26, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina ya Viongozi
wa Dola katika Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali Madini baada ya
kuifunga semina hiyo kwenye ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma, Januari
26, 2019. Waliokaa kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Madini,
Profesa. Simon Msanjila, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Mwanasheria Mkuu
wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.
Bilinith Mahenge na kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, Stanslaus
Nyongo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Friday, January 24, 2020
WAKALA WA VIPIMO (WMA) WATOA ELIMU KAMATI YA BUNGE VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (kulia) akizungumza wakati
wa semina iliyokuwa ikitolewa na Wakala wa Vipimo nchini kwa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, iliyofanyika jijini
Dodoma jana. Waziri Bashungwa amewaagiza Wakala wa Vipimo kuendelea
kujitangaza zaidi ili wananchi waweze kuwaelewa vizuri na hatimaye
Tanzania ya viwanda iweze kutusukuma kufikia uchumi wa kati. Kulia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na
Mazingira ambaye ni Mbunge wa Mvomero, Suleman Sadiki na katikati ni
Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira,
Zainabu Mkamba.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ambaye
ni Mbunge wa Mvomero, Suleman Sadiki (katikati walioketi) akifafanua
jambo kwa wajumbe wa kamati yake wakati Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Vipimo Dkt. Ludovick Manege (kushoto aliyesimama) alipokuwa akitoa
wasilisho mbele ya wabunge kamati juu ya utendaji kazi na majukumu ya
Wakala wa Vipimo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege akitoa
wasilisho mbele ya wabunge Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,
Biashara na Mazingira pamoja na kuelezea mafanikio ya miaka minne ya
serikali ya
Awamu ya tano. katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Viwanda, Biashara na Mazingira ambaye ni Mbunge wa Mvomero, Suleman
Sadiki na kulia ni Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,
Biashara na Mazingira, Zainabu Mkamba.
Baadhi ya wabunge wakichangia mada wakati wa semina iliyokuwa ikitolewa na Wakala wa Vipimo nchini kwa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira,
iliyofanyika jijini Dodoma jana.
Baadhi ya wajumbe kutoka Wakala wa Vipimo na Wizara ya Viwanda na Biashara wakifuatilia majadiliano wakati wa semina.
TFRA YAMKERA WAZIRI HASUNGA, ATAKA BEI YA MBOLEA ISHUKE
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi cha vyama vya ushirika kuhusu ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kilichofanyika katika ukumbi wa Mpendejirani eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 21 Januari 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga
(Mb) ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuhakikisha kuwa
inapanga na kusimamia bei elekezi za mbolea kwa lengo la kumuwezesha mkulima kupata
mbolea kwa bei nafuu.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza ulazima wa vyama vya ushirika kuagiza mbolea, wakati akifungua kikao kazi cha vyama vya ushirika kuhusu ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kilichofanyika katika ukumbi wa Mpendejirani eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 21 Januari 2020.
Amesema kuwa Kanuni za usimamizi na
uagizaji wa mbolea kwa pamoja zilitungwa kufuatia tafiti za kina zilizofanywa
na Watafiti wa ndani ya Nchi na wengine kutoka Taasisi za Kimataifa ambapo Matokeo
ya Tafiti hizo yalionesha kuwa BPS inaweza kupunguza gharama ya uagizaji wa mbolea
kwa zaidi ya asilimia 50.
Waziri
Hasunga ameyasema hayo tarehe 21 Januari 2020 wakati wa ufunguzi wa kikao kazi
cha vyama vya ushirika kuhusu ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kilichofanyika
katika ukumbi wa Mpendejirani eneo la Vwawa Mkoani Songwe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mkoani Songwe walioshiriki wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha vyama vya ushirika kuhusu ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kilichofanyika katika ukumbi wa Mpendejirani eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 21 Januari 2020.
Pamoja na Serikali kusisitiza wakulima kuvitumia Vyama vya
Ushirika katika utatuzi wa changamoto za kiuchumi na Kijamii, bado wanaushirika
wameshindwa kubuni mfumo madhubuti wa kuwaunganisha katika ununuzi wa Pembejeo
ambazo zingewapa unafuu wa gharama za uzalishaji pamoja na kwamba Sera ya
Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002, kusisitiza kwamba Ushirika ni chombo pekee
cha kumletea mwananchi mnyonge maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Lakini
pamoja na matarajio hayo ya serikali na wakulima nchini bado gharama za mbolea
sio rafiki kwa wakulima pamoja na bei kushuka mwaka 2019 ukilinganisha na miaka
iliopita.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi cha vyama vya ushirika kuhusu ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kilichofanyika katika ukumbi wa Mpendejirani eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 21 Januari 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo,
Songwe
Waziri Hasunga amewaeleza washiriki wa
mkutano huo kuwa Tayari Wizara ya Kilimo kupitia kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika
Tanzania imetoa Waraka wa kuagiza Vyama vyote vya Ushirika kupeleka mahitaji
yao ya mbolea kwenye Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ili iagizwe
kwa pamoja kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS – Bulk Procurement System).
Endapo Vyama vya Ushirika vitaagiza
mbolea kupitia BPS kwa kutumia dhamana za Benki (Bank guarantees) zenye tozo ndogo (asilimia 1 – 4) na kusafirisha mbolea kwa pamoja kwa njia ya reli,
gharama zitapungua na mbolea ya NPK itakuwa na bei ndogo kuliko DAP.
Amesema
Vyama vya ushirika vinapaswa kuwa ndio kimbilio la wakulima na hivyo kuagiza
mbolea kwa pamoja itapelekea kupungua kwa gharama za mbolea na ziweze kufika
kwa wakati.
Kadhalika,
katika mkutano huo Waziri Hasunga ameiagiza Taasisi ya Utafiti na
udhibiti wa Viuatilifu katika ukanda wa kitropiki TPRI kutoa
mafunzo kwa wananchi nchini kuhusu matumizi sahihi ya viuatilifu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe John Palingo akimuwakilisha mkuu wa
mkoa wa Songwe katika mkutano huo ameipongeza serikali kwa kuanzisha na
kuvisimamia vyama vya ushirika nchini kwani kupitia umoja huo wakulima
wameendelea kunufaika ikiwa ni pamoja na kuwa na bei nzuri ya mazao.
Thursday, January 23, 2020
TANZANIA YAONGOZA AFRIKA MASHARIKI KWA KUFIKISHA MIUNDOMBINU YA UMEME VIJIJINI - SUBIRA MGALU
NA K-VIS BLOG, Khalfan Said, Kisarawe
Naibu
Waziri wa Nishati amesema Tanzania inaongoza Afrika Mashariki kwa kujenga
miundombinu ya umeme vijijini.
Ameyasema
hayo akiwa katika ziara ya kukagua upelekaji wa umeme kwenye maeneo ya
pembezoni mwa Miji na Majiji (periurban)
Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani Januari 23, 2020. Serikali kupitia Wizara ya
Nishati inaendesha mradi wa periurban
kwa majaribio katika baadhi ya maeneo ya Wilaya za Kisarawe, Bagamoyo, Kibaha, Kigamboni na Ukonga jijini
Dar es Salaam ili kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo kutumia umeme kwa bei
nafuu ya shilingi elfu 27,000/= tu.
“Ilani
ya uchaguzi 2015/2020 ilisema umeme usambazwe vijijini na jumla ya vijiji 8,500
kati ya 12,268 sawa na asilimia 67 ya vijiji vyote Tanzania vimefikiwa na
miundombinu ya umeme.” Amefafanua Mhe. Mgalu ambaye katika ziara hiyo
alifuatana na Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani,
Mhandisi Hassan Said, Meneja wa TANESCO
Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Madulu na viongozi wengine.
Mradi
wa Periurban unapaswa kukamilika Juni
mwaka huu 2020, na licha ya changamoto za hapa na pale, Mhe. Naibu Waziri
amewahakikishia wakazi wa maeneo hayo kuwa miezi mitano kuanzia sasa wataanza
kuwasha umeme kwenye maeneo hayo.
Katika
Wilaya ya Kisarawe, jumla ya vijiji…………………..vitafaidika na mradi huo.
Amemtaka
mkandarasi wa mradi huo kampuni ya Sengerema kuhakikisha kazi inakamilika
katika kipindi cha miezi mitano kilichosalia na hakuna muda kuongezwa.
“Rai
yangu kwa mkandarasi ni kufanya kazi usiku na mchana hakuna kulala, na wale
suppliers wasambaza vifaa wa viwanda vya ndani vinavyozalisha nguzo, waya na
transfoma, mita wapeni ushirikiano wakandarasi ili waweze kumaliza kazi
zilizopo kwa wakati.” Alisisitiza Mhe.
Mgalu.
Mhe.
Mgalu alisema katika mradi huu wa majaribio wa periurban unalenga
kuwaunganishia umeme jumla ya wateja elfu 38,000 huku Wilaya ya Kisarawe na
Ukonga maeneo 62 yatafaidika.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo ameipongeza TANESCO
kwa kazi nzuri wanayoifanya Wilayani Kisarawe kuhakikisha huduma za upatikanaji
wa umeme inakuwa bora na kwamba ongezeko la kiwango cha umeme wilayani humo
litapelekea kuendelea kuing’arisha wilaya mbali na kuwafikishia umeme wananchi
kwenye maeneo mengi ya vijijini lakini pia utasaidia kuweka taa za barabarani
pia.Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, (kushoto) akipoz kwa picha na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Mhe. Jokate Mwegelo baada ya kupokea cheti cha shukrani kutoka kwa Mkuu huyo wa wilaya kwa ushiriki wake wa kuchangia kampeni ya "TOKOMEZA ZERO" inayolenga kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wilayani humo. Mhe. Mgalu alikuwa kwenye ziara ya kukagua upelekaji umeme kwenye maeneo ya pembezoni mwa miji na majiji (periurban) ambapo miongoni mwa maeneo yatakayofaidika na mradi huo ni taasisi za elimu.
Naibu Waziri akipokea cheti hicho kutoka kwa DC Mhe. Mwegelo.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, akipeana mikono na Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Hassan Said mara baada ya kuzungumza na wananchi kwenye shule ya sekondari Christon iliyoko nje kidogo ya Mji wa Kisarawe Mkoani Pwani Januari 23, 2020 wakati akikagua upelekaji wa umeme kwenye maeneo ya pembezoni mwa miji na majiji periurban
Mhe. Subira Mgalu (katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani Mhe. Jokate Mwegelo na viongozi wengine akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua upelekaji umeme kwenye maeneo ya pembezoni mwa miji na majiji (periurban) wilayani Kisarawe Januari 23, 2020.
Mhe. Mgalu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo.
TCAA YAWAJENGEA UWEZO KUPENDA SEKTA YA ANGA ZAIDI YA WANAFUNZI 600 WA SHULE ZA SEKONDARI MJINI TABORA
Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kituo cha Tabora Bw. Daniel Nyimbo akielezea jambo kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo. Zaidi ya wanafunzi 600 kutoka shule ya sekondari Mirambo, Tabora Boys na Tabora Girls wameshiriki Warsha hiyo.
Sehemu ya wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha hiyo wakisikiliza maelekezo kutoka kwa wataalamu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.
Mkufunzi Mkuu Kitengo cha huduma za viwanja vya ndege kutoka Chuo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) kilichopo Dar es Salaam Bi.Thamarat Abeid akitoa ufafanuzi wa fursa za kimasomo katika chuo hicho pamoja na sifa za ujumla zinazohitajika ili kujiunga na masomo ya usafiri wa Anga kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha hiyo.
Picha ya pamoja baada ya warsha.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Milambo wakijiandaa kushiriki warsha ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo.
Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kituo cha Tabora Bw.Daniel Nyimbo akielezea jambo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Milambo walioshiriki warsha ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo.
Mkufunzi Mkuu Kitengo cha huduma za viwanja vya ndege kutoka Chuo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) kilichopo Dar es Salaam Bi.Thamarat Abeid akitoa ufafanuzi wa fursa za kimasomo katika chuo hicho pamoja na sifa za ujumla zinazohitajika ili kujiunga na masomo ya usafiri wa Anga kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha hiyo.
Picha ya pamoja baada ya warsha.
Subscribe to:
Posts (Atom)