Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wananchi wa Mji wa Mbalizi mkoani
Mbeya kujikita katika kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kutatua
changamoto zinazowakabili.
Dkt. Ndugulile ameyasema hayo mjini Mbalizi mkoani Mbeya
alipokuwa akishiriki katika ujenzi wa vyumba tisa vya Madarasa ya Shule ya
Sekondari Utengule Usongwe kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vyumba vya
madarasa.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali inaendelea kuamsha ari ya
wananchi katika kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuwaunga mkono pale
wanapoanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao.
"Wizara hii inahusika na masuala yote ya maendeleo ya kazi
yetu kubwa ni kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea na kushiriki katika
shughuli za maendeleo" alisema Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali ya Awamu ya tano inataka
kuona wananchi wanafanya kazi wanajishugulisha na shughuli za mendeleo kwa
kuchangia katika miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia ramani ya jengo la mama na mtoto
katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kitengo cha Mama na Mtoto.
|
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Bw. Benedict Mahenge ameishukuru
Serikali wananchi na wadau walijitolea katika kuchangia ujenzi wa vyumba vya
madarasa katika shule hiyo kwani itasaidia kupunguza adha ya wanafunzi kukaa
wengi katika darasa moja.
Aidha Afisa Elimu Kata ya Utengule Usingwe George Mtawa amesema
ujenzi wa vyumba vya madarasa tisa umekuja kutokana na kuwa na idadi kubwa ya
shule za msingi na ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba hivyo wananchi
waliamua kuanza ujenzi huo ili kuondokana na changamoto ya watoto kukosa
madarasa ya kusomea.
Naye Diwani wa Kata ya Utengule Usongwe Elia Mkono amesema kuwa
wananchi wa Kata hiyo wameamua kujenga vyumba vya madarasa hayo ili kuhakikisha
watoto 981 wanapata madarasa ya kuanza kidato cha kwanza katika Shuke hiyo.
No comments:
Post a Comment