Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) na wenzao wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani
wakimfanyia mgonjwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanyakazi (ECHO
Cardiograph) mara baada ya kumaliza kumfanyia mgonjwa upasuaji mkubwa wa
kubadilisha valvu ya moyo iliyokuwa haifanyi kazi kwenye kambi maalum ya upasuaji wa moyo ya siku 12 kwa
watoto na watu wazima inayoendelea katika Taasisi hiyo. Hadi sasa wagonjwa 15
ambao ni watu wazima saba na watoto nane wameshafanyiwa upasuaji na hali zao
zinaendelea vizuri.
Madaktari
bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na
wenzao wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani
wafanya upasuaji mkubwa wa moyo wa kubadilisha valvu, kupandikiza na
kurekebisha mishipa ya damu ya moyo kwa wagonjwa 15 katika kambi maalum
ya upasuaji wa moyo kwa watoto na watu wazima inayoendelea katika
Taasisi hiyo
|
No comments:
Post a Comment