Matokeo chanyA+ online




Tuesday, January 14, 2020

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI WA AFRIKA KUSINI, ZIMBABWE, NAMIBIA NA NIGERIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kuwaapisha Mabalozi wapya  wanne walioteuliwa kuwaikilisha Tanzania katika nchi  mbalimbali walizopangiwa . Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020

Rais  Dkt. John Magufuli  tarehe 14 Januari, 2020 amewaapisha Mabalozi 4 aliowateua hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Afrika Kusini, Namibia, Zimbabwe na Nigeria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mabalozi wapya  wakila kiapo cha maadili kwa watumishi wa Umma  mbele ya Kamshna wa Maadili Jaji Mstaafu Haroid Nsekela mara baada ya kuwa apisha kuwaikilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa . Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020

Walioapishwa ni Mej. Jen (Mstaafu) Gaudence Salim Milanzi anayekuwa Balozi wa Tanzania Pretoria - Afrika Kusini, Dkt. Modestus Francis Kipilimba anayekuwa Balozi wa Tanzania Windhoek – Namibia, Prof. Emmanuel David Mwaluko Mbennah anayekuwa Balozi wa Tanzania Harare – Zimbabwe na Dkt. Benson Alfred Bana anayekuwa Balozi wa Tanzania Abuja – Nigeria.
Mabalozi wakila kiapo

Baada ya kuwaapisha, Mhe. Rais Magufuli amewataka kuripoti katika vituo walivyopangiwa ndani ya wiki 2 kuanzia sasa na amewasisitiza kwenda kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kwa kuzingatia maslahi ya Taifa hasa kiuchumi na kuwawezesha Watanzania kupata ajira katika fursa zilizopo katika nchi hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kuwaapisha Mabalozi wapya  wanne walioteuliwa kuwaikilisha Tanzania katika nchi  mbalimbali walizopangiwa . Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amewataka Mabalozi hao kufuatilia maeneo yote ambayo Mhe. Rais Magufuli alikubaliana na Waheshimiwa Marais wenzake alipotembelea nchi hizo hivi karibuni, na pia kuitangaza vyema Tanzania ambayo kwa sasa inapiga hatua kubwa katika maeneo mengi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na  Mabalozi wapya  wanne walioteuliwa kuwaikilisha Tanzania katika nchi  mbalimbali walizopangiwa  mara baada ya kuwaapisha Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Hafla ya kuapishwa kwa Mabalozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
 Mabalozi wapya  wakila kiapo cha maadili kwa watumishi wa Umma  mbele ya Kamshna wa Maadili Jaji Mstaafu Haroid Nsekela mara baada ya kuwa apisha kuwaikilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa . Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Add caption
Kabla ya kuwaapisha Mabalozi hao, Mhe. Rais Magufuli ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya  wanne walioteuliwa kuwaikilisha Tanzania katika nchi  mbalimbali walizopangiwa  mara baada ya kuwaapisha Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020



Picha na Ikulu







No comments:

Post a Comment