Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani (UTU ) Mwalimu Bi.Venessa Upendo Fölsenakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt.Abdallah Possi |
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani (UTU ) Mwalimu
Bi.Venessa Upendo Fölsen siku ya jumamosi aliongoza kamati ya uongozi wa
umoja huo katika kikao cha kukutana na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mheshimiwa Dkt.Abdallah Possi katika ubalozi wa Tanzania mjini
Berlin,ambako ubalozi uliwakaribisha kwa mikono miwili na kufanya
mazungumzo nao ambayo Kiongozi wa umoja wa Tanzania Ujerumani amelezea
kuwa Umoja huo utaitangaza Tanzania nchini ujerumani kwa nguvu zote kwa
maslahi ya Tanzania na watanzania,ususani katika sekta ya
Utalii,uwekezaji,afya na elimu ni mojawapo ya mambo yakatayopewa kipau
mbele,Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani ndio mwamvuli pekee
unawakusanya watanzania waishio nchini ujerumani na moja ya niya yake ni
kuleta mshikamano wenye kuleta maslahi kwa watanzania ujerumani na
nyumbani Tanzania.
Pia kwa upande wake Balozi Dkt. Abdallah
Possi amewataka watanzania kuungana pamoja kwa maslahi yao na ya
Tanzania,pia kujivunia utanzania wao kwa kuitangaza vema Tanzania katika
nyanza zote na vivutio vyake katika tufe la dunia ili kufanikisha
Tanzania ya Viwanda itakayokuza uchumi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani (UTU ) Mwalimu Bi.Venessa Upendo Fölsen |
No comments:
Post a Comment