Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala
ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki ametembelea na kukagua mazingira ya
uendeshaji wa kiwanda cha vifaa vya ujenzi cha SHAFA na kupongeza uzalishaji wa
tofali kiwandani hapo na kusema ni wa kuridhisha.
Ametoa pongezi hizo alipotembelea kiwandani Januari 20, 2020 ikiwa ni sehemu ya ziara yake
ya kikazi katika Mkoa wa Pwani ili kukagua mazingira ya wawekezaji, kusikiliza na kutatua changamoto
zinazowakabili ili kuendelea kuwa na mazingira mazuri ya wafanya biashara na
wawekezaji nchini.
Aidha katika ziara yake aliambatana na Watendaji kutoa Ofisi
yake, Uongozi wa Mkoa wa Pwani, Watendaji kutoka Wilaya ya Mkuranga pamoja na watendaji
wa Taasisi za Serikali ikiwemo TANESCO, TARURA, TRA, na Kituo cha Uwekezaji
nchini (TIC).
Akizungumza na waandishi wa habari kiwandani hapo, alisema
amevutiwa na uwekezaji katika kiwanda hicho kwa kuwa na matofali bora kwa
kuzingatia muhimu wa mahitaji ya ujenzi katika kuhakikisha kuna kuwa na majengo
bora, kiasa na imara kwa matumizi mbalimbali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika ziara yake ya kikazi katika kiwanda cha kutengeneza matofali cha SHAFA kilichopo Wilaya ya Mkuranga Pwani |
“Vipo viwanda zaidi ya vitatu vinavyotengeneza tofali nchini
ingawa hiki kinaongoza kwa kuwa na mitambo ya kisasa aina ya MASA yenye uwezo wa kuzalisha tofali 10,000,
vigae vya sakafuni zaidi ya 10,000 kwa
siku ukilinganisha na viwanda vingine na kwa nchi za Afrika Mashariki ni kiwanda
cha mfano kwa kutoa matofali yenye ubora wa hali ya juu,”alesisitiza Waziri
Kairuki.
Alieleza kuwa, ipo haja ya kuunga mkono jitihada za
wawekezaji wa viwanda kama hivyo ili kuendelea kujieletea maendeleo ya nchi kwa
ujumla kwa kuzingatia mchango wake katika ngazi zote kuanzia Kijiji, Taifa hadi
nje ya nchi.
Aliongezea kuwa , furaha yake ni kuona kiwanda kinaweza kuzalisha
kwa haraka, ubora na idadi kubwa kwa siku ili kuhakikisha kuna kuwa na majengo
salama na yenye kudumu hadi vizazi vijavyo.
Akiwasilisha taarifa ya kiwanda kwa waziri, Afisa Mahusiano wa
kiwanda hicho Bw. Agrey Roodluck alieleza malengo ya mradi ni pamoja na kuongeza
wigo katika sekta ya ujenzi kwa kuzingatia uzalishaji wake unalenga kuwa na
aina tofauti tofauti za matofali yenye ubora na kuweza kukidhi mahitaji kwa
gharama nafuu.
“Mradi umezingatia changamoto zilizopo za ukosefu wa matofali
bora katika maeneo mengi yanayohitajika katika ujenzi wa maegesho ya magari,
bararaba, maeneo ya viwanja vya ndege pamoja na majengo makubwa na madogo,”alieleza
Roodlucky
Aidha alitoa omba kwa waziri kuendelea kuhamasisha ujenzi
salama wa majengo ya taasisi, nyumba ndogo na kubwa kwa kuendelea kutumia
tofali za kiwanda hicho na kueleza kuwa ni sehemu ya kuunga mkono maendeleo ya
nchi kwa kuzingatia malighafi zinazotumika zinatoka nchini.
“Hadi kukamilika kwa mradi huu utatumia jumla ya Tshs Bilioni
15.3 na tayari zaidi ya asilimia 90 zimeshatumika
na asilimia 99.9 za malighafi za kiwanda zinatoka hapa hapa nchini ikiwemo saruji,
mchanga, kokoto na maji,”alisisitiza
Sambamba na hilo alisema, lengo kuhakikisha kiwanda kinatoa
mchango katika pato la taifa katika kuhakikisha kinalipa kodi zote zinazotakiwa
na kuendelea kuzalisha ajira zaidi ya 100 zitakazozingatia kundi kubwa la
vijana wazawa ili kuweza kuendesha mitambo iliyopo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga alimshukuru
waziri kwa kutembelea mradi huo, na kueleza kuwa, ni mradi wenye faidi katika
Wilaya yake kwa kuzingatia mchango wa mradi na namna walivyojikita katika
kuhakikisha wanakuwa wenye bidhaa bora na kukidhi mahitaji ya wateja wake.
No comments:
Post a Comment