Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent
Bashungwa azindua kliniki ya Biashara Zanzibar. Tukio hili lilishuhudiwa na
Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe Balozi Amina Salum Ali. Huduma ya Kliniki ya
Biashara inalenga kutatua changamoto za
biashara kwa wafanyabiashara kwa kuwahudumia ana kwa ana. Huduma hii hujumuisha
taasisi zote za kimkakati katika kusaidia mnyororo wa biashara. Huduma ya
Kliniki ya Biashara ilianzishwa na inasimamiwa na TanTrade
|
No comments:
Post a Comment