Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, amesema Wananchi wa Tanzania wameungana na Wananchi wa Oman katika
maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mfalme wa Nchi hiyo Hayat Sultan Qaboos bin
Said.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo wakati
alipokuwa akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Ali Almahroqi
alipofika kwenye Ofisi za Ubalozi huo Mikocheni Jijini Dar es Salaam kwa ajili
kutia saini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Sultan Qaboos
bin said kilikchotokea mwanzoni mwa wiki.
Akizungumza na Balozi Ali Almahroqi
kwa Masikitiko Makamu wa Rais alisema amepokea kwa Mstuko mkubwa taarifa ya
kifo cha Sultan Qaboos bin Said aliyefariki tarehe 10 Januari 2020 akiwa na
umri wa miaka 79 hivyo Wananchi wote wa Tanzania wanaungana na ndugu zao wa
Oman kwenye kuomboleza msiba huo na Mungu ailaze Roho ya Marehemu Sultan
Qabbos Peponi Amin.
Aidha Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan, amemtakia kila la heri kiongozi mpya wa Taifa hilo la Oman
Sultan Haitham bin Tariq Al Said katika kuwaongoza Wananchi wa Oman.
Nae Balozi wa Oman Nchini Tanzania
Mhe. Ali Almahroqi amemhakikishia Makamu wa Rais kwamba Nchi yake itaendelea
kuimarisha Uhusiano wa Undugu uliokuwepo tokea enzi na enzi.
|
No comments:
Post a Comment