|
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas
Ndumbaro (aliyevaa miwani) akiwasilisha taarifa ya utendaji wa Wizara kwa kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika ukumbi wa Bunge
jijini Dodoma
|
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki imewasilisha taarifa ya utendaji kazi wake kwa kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na kusema Serikali ina
mpango wa kujenga bandari ndogo katika ziwa Tanganyika mpakani mwa Tanzania na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema hayo
alipowasilisha taarifa taarifa ya Utekelezaji wa Wizara ya mwezi Juni
hadi Desemba 2019 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
|
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (aliyevaa miwani)
akiwasilisha taarifa
ya utendaji wa Wizara kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi
“Mhe. Mwenyekiti, ili kunufaika kiuchumi
kupitia DRC, tumepanga kujenga bandari ndogo katika Ziwa Tanganyika na kufungua
Ubalozi mdogo katika mji wa Lubumbashi, mji huu uko umbali wa kilomita 3000
kutoka jijini Kinshasa,” alisema Dkt. Ndumbaro.
Amesema ujenzi wa bandari ndogo eneo la
mpakani katika Ziwa Tanganyika kutawezesha bidhaa zinazozalishwa Tanzania
kwenda nchini humo kiurahisi kuliko ilivyo sasa ambapo wafanyabiashara
wanapitisha biashara zao nchini Zambia hadi kufika nchini DRC.
|
|
Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Mussa
Azzan Zungu (kushoto) akisikiliza taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Dkt. Ndumbaro.
|
Aidha amesema Serikali inachukua hatua
mbalimbali katika maeneo ya mpaka na nchi hiyo ikiwemo kuhakikisha amani na usalama vinaimarishwa
ili wananchi wa pande zote mbili wafanye biashara bila hofu yoyote.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Mussa Azzan
Zungu imekutana na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki jijini Dodoma na kupata taarifa mbalimbali za utendaji wa
Wizara.
Mhe. Zungu amesisitiza umuhimu wa
Tanzania kushirikiana na DRC katika kuhakikisha amani na usalama vinaimarika
hata baada ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa (MONUSCO) kumaliza
muda wake nchini humo.
No comments:
Post a Comment