Waziri
wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema Serikali imedhamiria kupeleka umeme wa
gridi ya Taifa katika Mkoa wote wa Kagera, awamu kwa awamu ikianza na Wilaya za
Bukoba Vijijini, Muleba na Misenyi.
Amesema
Wilaya hizo za awali zitaungwa kwenye gridi ya Taifa ndani ya kipindi cha mwezi
mmoja kutoka sasa.
Waziri
ameeleza hayo Februari 27 mwaka huu wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa
Kagera, Brigedia Generali Marco Gaguti, akiwa katika ziara ya kazi.
“Wataalamu
wetu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wataanza kujenga njia ya
kusafirisha umeme wa kilovoti 33 kutoka Kanazi mpaka Itako na kutoka Itako
mpaka Misenyi,” amefafanua.
Akieleza zaidi,
amesema maeneo hayo yataanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa inayotoka Geita
mpaka maeneo ya Ngara, Biharamulo na baadaye Misenyi.
Hata
hivyo, Waziri amesema maeneo ambayo hayatafikiwa katika awamu ya kwanza
kikiwemo kiwanda cha sukari cha Kagera na mengine yote yatakayosalia,
yataendelea kutumia umeme kutoka nchi jirani ya Uganda wakati wakisubiri awamu
nyingine ya utekelezaji wa mpango huo.
Akielezea
kuhusu kuyaunga maeneo hayo yatakayosalia, Waziri amesema zoezi hilo
litafanyika baada tu ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya umeme ya Kakono,
Rusumo na Nyakanazi.
“Miradi
hiyo ikikamilika, taratibu tutaweza kuwaondoa wale waliosalia kutoka kwenye
gridi ya Taifa upande wa Uganda na kuwaunga kwenye gridi ya Taifa ya hapa
nchini.”
Aidha,
Waziri amebainisha kuwa, utekelezaji wa mpango huo ni sehemu ya mkakati wa
serikali unaoendelea ukilenga kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika
maeneo yote ya nchi yetu.
Akielezea
kuhusu kuyaunga maeneo hayo yatakayosalia, Waziri amesema zoezi hilo
litafanyika baada tu ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya umeme ya Kakono,
Rusumo na Nyakanazi.
“Miradi
hiyo ikikamilika, taratibu tutaweza kuwaondoa wale waliosalia kutoka kwenye
gridi ya Taifa upande wa Uganda na kuwaunga kwenye gridi ya Taifa ya hapa
nchini.”
Aidha,
Waziri amebainisha kuwa, utekelezaji wa mpango huo ni sehemu ya mkakati wa
serikali unaoendelea ukilenga kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika
maeneo yote ya nchi yetu.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Ujumbe wake, wakikagua kituo cha kupoza umeme Kyaka, kilichopo wilayani Misenyi, Mkoa wa Kagera, alipokuwa katika ziara ya kazi Februari 27 mwaka huu. |
Veronica Simba –
Kagera
Ameeleza
zaidi kuwa, mbali ya kuimarisha hali ya upatikanji umeme nchini, serikali pia
inapanga kuwa na umeme mwingi utakaotosheleza mahitaji ya ndani na kuuza ziada
kwa nchi jirani za Ukanda wa Afrika Mashariki.
“Leo sisi
tunanunua umeme kutoka kwa jirani zetu. Tunataka nasi tuwauzie umeme hapo
baadaye. Uhakika wa kufanya hivyo tunao kutokana na miradi mikubwa tunayoitekeleza
ukiwemo ule wa kuzalisha umeme (megawati 2,115) wa Julius Nyerere huko Rufiji.”
Kwa upande wake,
Brigedia Gaguti amepongeza uamuzi huo wa serikali kuunganisha umeme wa gridi ya
Taifa katika Mkoa wote wa Kagera na kuahidi kutoa ushirikiano kadri utakavyohitajika
katika kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kikamilifu.
Katika ziara
hiyo ya siku moja, Waziri na Ujumbe wake walitembelea maeneo mbalimbali ambayo
yatahusika katika utekelezaji wa Mradi huo kikiwemo kituo cha kupoza umeme cha
Kyaka kilichopo wilayani Misenyi.
No comments:
Post a Comment