Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile |
Na
Englibert Kayombo, WAMJW, Arusha
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile amewahakikisha Watanzania kuwa nchi bado iko salama na hakuna mgonwjwa
yeyote mwenye ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Dkt
Ndugulile ametoa kauli hiyo akiwa Jijini arusha katika Ziara zake za kikazi
ambapo waandishi wa habari walimuuliza juu ya tetesi za uwepo wa ugonjwa huo
nchini, pamoja na kutaka kufahamu ukweli wa taarifa za mtu anayedai kuwa na
dawa za ugonjwa huo.
“Niseme
tuu kuwa Tanzania mpaka sasa hivi bado tuko salama na hakuna mgonjwa
yeyoteambaye ameripotiwa na amethibitika kuwa na ugonjwa” amesema Dkt
Ndugulile.
Amesema
kuwa Serikali imekuwa ikifuatilia taarifa mbalimbali za washukiwa na watu wote
ambao tunawahisi kuwa na ugonjwa huo na tumeweza kuwapima na kubaini kuwa
hawana ugonjwa.
“Sambamba
na hilo tumeendelea kuchukua tahadhari mbalimbali na mimi niko katika Mkoa huu
wa Arusha na nitaenda Kilimanjaro kwenda kuangalia utayari” amesmea Dkt.
Ndugulile na kuendelea kusema “ Nimepita hapa leo nimeongea na uongozi na
nimeridhika na maandalizi ambayo tunayo hapa katika Mkoa huu wa Arusha katika
kudhibiti ugonjwa huo” Ameeleza Dkt. Ndugulile
Akijibu
kuhusu mtu ambaye anasema kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo ambaye
anajulikana kwa jina la Mosses Mollel maarufu kwa jina la “Nabii namba saba”
aliyetoa taarifa za kuwa na dawa yenye uwezo wa kutibu virusi vya corona, Dkt
Ndugulile amesema kuwa anazo taarifa za mtu huyo ambazo zimesambaa kwenye
mitandao ya kijamii na vyombo vya habari akijitangaza kuwa anayodawa ya kutibu ugonjwa huo na kumtaka athibitishe kauli yake.
“Kimsingi nimeiona hiyo taarifa ya
huyo mtu anayejiita Nabii Saba kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa wa
Corona ,ila hapa kwetu Tanzania hatuna maambukizi yoyote ya ugonjwa huyo
,tunachotaka huyo mtu atuthibitishie uwezo wake wa kutibu huo ugonjwa wa
Corona” Amesema Ndugulile
Ameongeza kuwa iwapo atashindwa
kuthibitisha atachukuliwa hatua Kali za kisheria.
Amesema hadi sasa Serikali imetuma
wataalamu wake kwenda kumsaka na kumhoji kama anavyo vibali Vya kutoa huduma ya
Tiba na kujitangaza kuwa anatoa Huduma ya kutibu ugonjwa huo hatari ambao
hadi sasa mataifa bado yanahaha kusaka Tiba ya ugonjwa huo.
Nabii Namba Saba ambaye ni mkazi wa
Ngaramtoni Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha amekuwa akijitangaza kuwa anayo dawa
ya kutibu ugonjwa huo wa virusi vya corona na kuweka mawasiliano yake
kwenye mitandao .
Dkt.
Ndugulile amesema kuwa mtu yeyote anayetoa tiba asili na mbadala kwanza ni
lazima asajiliwe na mamlaka husika ambayo ni Wizara ya Afya, pili lazima dawa
zake ziwe zimesajiliwa na Wizara ya Afya na kusisitiza kuwa nabii huyo pia
anapaswa kuthibitisha amesajiliwa wapi na lini.
“Tuepuke
kutoa kauli ambazo zinakwenda kuchanganya jamii, na endapo tutabaini mtu huyu
hana sifa ambazo anasema kuwa nazo tutamchukulia hatua za kisheria” Amesema
Dkt. Ndugulile.
No comments:
Post a Comment