Tanzania
imesema hatua zote ambazo zimechukuliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kwa kufanya mabadiliko katika sheria za vyama vya
siasa,sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali na ile ya vyombo vya
habari ina lengo la kuimarisha uwajibikaji na uwazi pamoja na
kuhakiskisha misingi na tunu za Taifa zinaheshimiwa na kuendelezwa.
Akihutubia
katika Kikao cha 43 cha Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa
linaloendelea Geneva nchini Uswisi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kuwa
Tanzania inaheshimu na itaendelea kuheshimu haki zote binadamu zikiwemo
za kisiasa na kwamba sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania zina lengo jema la kuhakikisha Tanzania inabaki
kuwa Taifa lenye amani,umoja na utulivu.
Pia
Prof. Kabudi ameifahamisha jumuiya ya Kimataifa kuwa mwaka huu Tanzania
itafanya uchaguzi wake mkuu wa sita tangu kuanzishwa kwa vyama vingi
vya siasa na kuihakikishia jumuiya hiyo kuwa uchaguzi huo utakuwa wa
uwazi,huru na wa haki na kwamba Tanzania itaalika waangalizi mbalimbali
wa uchaguzi watakaotaka kushuhudia namna Watanzania wanavyotekeleza moja
ya haki zao za msingi katika suala la kidemokrasia kwa kuchagua
viongozi wao.
Amesema
Tanzania inaheshimu na itaendelea kutekeleza kwa vitendo haki zote za
binadamu bila ubaguzi na kwamba madai yanayoishutumu Tanzania kukiuka
haki za binadamu ni propaganda na haswa zinatokana na hatua kali
zinazochukuliwa dhidi ya rushwa,ubadhirifu wa mali za umma,madawa ya
kulevya,uzembe katika ofisi za umma pamoja na hatua zinazochukuliwa
kulinda rasilimali na maliasili ya Tanzania kwa manufaa ya Watanzania.
Mradi
huo umelenga kuangalia takwimu mbalimbali zinazohusu biashara kwa
kuangalia nchi ambazo Tanzania inaagiza ama kuuza bidhaa zake kwa wingi
katika nchi za Jumuiya ya Madola mradi ambao umeelezwa kuwa na manufaa
makubwa kwa Tanzania ambapo kwa sasa nchi za India na Afrika kusini
ndizo kinara.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi Patricia Scotland
amesema Tanzania ni mdau muhimu katika jumuiya hiyo na kwamba amefurahi
kumkabidhi Prof. Kabudi nakala ya utafiti huo kwa niaba ya Tanzania
jambo litakaloifanya Tanzania kuendelea kuangalia maeneo ya kujiimarisha
katika ufanyaji wa biashara na nchi za Jumuiya ya Madola.
Mbali
na masuala hayo ya mradi huo wa takwimu wa biashara kuhusu Tanzania
uliofanywa bure na Jumuiya hiyo ya Madola pia wawili hao wamezungumzia
masuala mengine ikiwa ni pamoja na namna Jumuiya hiyo na Tanzania
zitakavyofanya kuongeza usawa wa jinsia,masuala ya haki za binadamu
pamoja na uimarishaji wa mfumo wa mahakama nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment