|
Msanii Shetta na G Nako wakitumbuiza eneo la Mlowa Mbozi Mkoani Songwe wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipokuwa Mkoani hapo.Uwepo wa kipato katika familia hasa mwanamke akiwezeshwa kiuchumi inapunguza kuwepo kwa vitendo vya ukatili katika jamii zetu.
Hayo
yamebainishwa Mlowa Mkoani Songwe na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara
Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha wakati msafara wa
kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia uliposimama Mkoani hapo.
Amesema
kuwa Serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili imeanzisha mpango
mkakati wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto
uliozinduliwa mwaka 2017/2018 na kumalizika mwaka 2021/2022. | |
|
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Happy Msimbe akielezea masuala ya kisheria wakati wa msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipokuwa Mkoani hapo."Serikali
inawezesha wananchi kiuchumi hasa wanawake katika Halmashauri zetu na
taasisi za fedha wananchi tuchangamkie fursa hii" alisema
Bi.
Imelda amewasihi wanaume kuwapa ushirikiano wanawake katika kuhakikisha
wanaweza kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili waweze kuchangia
maendeleo ya familia, jamii na Taifa.
Akizungumzia masuala ya
Kisheria Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Happy Msimbe amesema Serikali inasimamia Sheria
mbalimbali katika kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo Sheria ya
Mtoto ya mwaka 2009 inayomlinda mtoto. |
|
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha akieleza namna Serikali inavyowawezesha wananchi kuondokana na vitendo vya ukatili wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipokuwa Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe. |
"Sheria zinasimamiwa ipasavyo nitoe wito kwa wananchi kutoa taarifa za vitendo vya ukatili vinavyotokea katika jamii zetu" amesema.
Ameongeza kuwa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inapewa nguvu na Sheria nyingine zinazosaidia kuwezesha watoto kupata haki zao za msingi zitakazosaidia kuboresha ustawi wao.
No comments:
Post a Comment