Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack
Kamwelwe akisisitiza jambo katika kikao cha Kamati ya Bunge ya
Miundombinu ambapo Wizara yake imewasilisha Taarifa ya utekeleaji ya
bajeti ya sekta ya uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na makadirio
ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Kikao hicho
kimefanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu
wakiwa katika kikao cha kamati ambapo wamepokea na kujadili Taarifa ya
utekeleaji ya bajeti ya sekta ya uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2019/2020
na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Kikao
hicho kimefanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
PICHA NA OFISI YA BUNGE
No comments:
Post a Comment