Matokeo chanyA+ online




Monday, March 23, 2020

KILOMITA 39 ZA BARABARA ZA LAMI ZAANZA KUJENGWA MJI WA SERIKALI MTUMBA DODOMA

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack  Bandawe akionesha kazi ya ujenzi wa barabara za lami inavyoendelea
 

Na Mwandishi Wetu
Ujenzi wa barabara za lami katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma  waanza kwa kasi ili kuimarisha mawasiliano na huduma kwa wananchi.
Akizungumza leo Machi 20, 2020 katika mahojiano maalum, Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack  Bandawe amesema kuwa ujenzi huo  unahusisha barabara zenye urefu wa kilomita 39 ndani ya mji huo.
“Serikali inaimarisha miundombinu ndani ya mji wa Serikali ikiwemo ujenzi wa barabara  za njia mbili zenye urefu wa kilomita 28 na zenye njia 4 kilomita 11, ujenzi huu unaenda sambamba na kujengwa kwa miundombinu mingine kama TEHAMA, Afya, Makazi na Sehemu za Biashara”, Alisisitiza Bandawe
Akifafanua  Bandawe amesema kuwa  ujenzi wa miundombinu katika mji wa Serikali unaenda sambamba kujengwa kwa majengo ya gorofa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi za Wizara 22.
Mji wa Serikali ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli mwezi Machi 2019.


Eneo lililosafishwa tayari kwa ujenzi wa barabara za lami katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma

No comments:

Post a Comment