 |
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana kwa Ishara na Viongozi wa Mkoa wa Pwani alipowasili katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha Pwani March 14,2020 kwa ajili ya kuongoza Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi na ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani. Jumla ya Shilingi Milioni zimechangishwa kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi huo.
Makamu
wa Rais na mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Samia Suluhu pamoja na
Rais mstaafu Jakaya Kikwete wameungana na wadau , kwenye harambee ya
kuchangia zaidi ya sh.milioni 500 ili kukamilisha ujenzi wa ukumbi wa
CCM mkoani Pwani,":ambapo ameeleza chama hicho mkoa sio maskini badala
yake waviendeleze vitega uchumi walivyonavyo.
Katika
harambee hiyo, imeweza kupatikana kiasi cha sh.milioni 584.1 ikiwa
fedha taslim milioni 113.4,ahadi milioni 471.6,mifuko ya saruji 400 na
ndoo za rangi 50.
Akizungumza
katika harambee hiyo iliyofanyika mjini Kibaha,Samia alieleza alisema
ofisi yake inachangia milioni kumi na kudai ,jengo hilo lilisuasua kwa
kipindi kirefu lakini chini ya usimamizi wake atasimamia ujenzi huo na
hakuna fedha wala nondo zitakazopotea kama zilivyopotea wakati huo.
|
 |
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno akimkabidhi Tuzo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua mchango wake mkubwa kwenye Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega uchumi la CCM Mkoa wa Pwani uliofanyika March 14,2020 Kibaha Mjini.
Alisema,
CCM Pwani ina vitega uchumi ,lakini waache kubakia kuvihesabu kwa namba
,wasilale badala yake waviendeleze ili kupiga hatua kiuchumi na
kuondokana na hali ya kuwa omba omba.
"Sisi
sio masikini wa namna hiyo, tuliendekeza matumbo kuliko lililo mbele
yetu, sasa tuache kuendekeza matumbo tufanye kazi,mkoa wa Pwani hauna
sababu ya kupita kuombaomba, maana mna mtaji lakini pia mmelala"
"Tujipange vizuri, itabakia tunasema hiki chetu,kile chetu lakini hamviendelezi"alibainisha Samia.
Samia
alifafanua, wahakikishe jengo hilo linakamilika mwezi June mwaka huu
ili kuondokana na kupanga ukumbi wakati wa shughuli za chama.
|

Nae ,Jakaya Kikwete alishukuru na kufurahi kwa kualikwa kwenye shughuli hiyo,na atachangia mifuko 200 ya saruji.
Jakaya
alisema ,wazo la ujenzi huo lina historia kwake, lilianza miaka mingi
,":Nimefurahi sana kuona msukumo wa kuendeleza vitega uchumi hivi
ambavyo vilisuasua lakini sasa vinaendelezwa kwa manufaa ya
chama."alisema Jakaya.
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,aliwaomba ,wadau na wananchi kuendelea kuchangia ili kutimiza adhma hiyo.
"Tumepewa
muda ,hadi mwezi June mwaka huu ,ujenzi uwe umekamilika hivyo juhudi za
pamoja zinatakiwa ili tukamilishe kwa wakati huo"alifafanua Ndikilo.
Katika
harambee hiyo, mfanyabiashara Bakhresa amechangia kiasi cha sh.milioni
100,Shubash Patel anaezeka jengo zima kwa gharama ya milioni 250.
Mkuu
wa mkoa wa Pwani Ndikilo alitoa sh.milioni 50,kamati ya siasa mkoa
mifuko 200 ya saruji na sh.milioni nne,wabunge 13 wa mkoa huo
wamechangia sh.milioni 16,ambapo rafiki wa mbunge wa viti maalum Zainab
Vullu amechangia milioni 10.
 |
Mhandisi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani Suleiman Nassor akimuelezea Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuhusu Jengo hilo litakavyokuwa wakati Makamu wa Rais alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo hilo March 14,2020 Kibaha Mjini. |
 |
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza Jambo kwa Viongozi wa Mkoa wa Pwani kuhusu Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo hilo Kibaha Mjini March 14,2020.kulia ni Rais Mstaafu awamu ya Nne Mhe. Jakaya Kikwete. |
 |
Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Ali Makoa akimuelezea Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuhusu litakavyokuwa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani litakapokamilika alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo hilo March 14,2020 Kibaha Mjini. |
 |
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi, Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa Mkoa wa Pwani kwenye Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani iliyofanyika March 14,2020 katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha Mjini. Jumla ya shilingi Milioni zimechangishwa kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi huo. |
 |
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM
Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza Jambo kwa
Viongozi wa Mkoa wa Pwani kuhusu Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la
Kitega uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani alipotembelea kuangalia Maendeleo ya
Ujenzi wa Jengo hilo Kibaha Mjini March 14,2020.kulia ni Rais Mstaafu
awamu ya Nne Mhe. Jakaya Kikwete. |
 |
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Kikwete akizungumza kwenye Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi na Ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani iliyoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Kibaha Mjini March 2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) |
 |
Jengo la Ofisi na ukumbi la Kitega Uchumi wa CCM Mkoa wa Pwani. Jumla ya Shilingi Milioni zimechangishwa kwa ajili ya kukamilisha Ujenzi huo. |
No comments:
Post a Comment