 |
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Halmashauri Mbulu Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, imefanya
ukaguzi na kuridhishwa na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya
ya Mbulu, inayojengwa katika kata ya Dongobesh wilayani Mbulu.
Akieleza
kuridhishwa kwake na hatua ya ujenzi na matumizi sahihi ya fedha za
Serikali, Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt, Jason Rweikiza amesema Kamati
ya Bunge imeridhishwa na hatua ya ujenzi kwa kuzingatia ubora na thamani
ya fedha zilizotolewa na Serikali, na kuitaka Ofisi ya Rais TAMISEMI,
kuhakikisha fedha zilizotengwa kwenye bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya
Hospitali hiyo zinatolewa haraka ili kukamilisha miundombinu iliyobaki
ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyokusudiwa. | | |
 |
Mwenyekiti
wa Kamati Dkt Jason Rweikiza na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga na kamati wakati wa ukaguzi |
 |
Mbunge
wa Manyoni Mashariki Mhe Daniel Mtuka(aliyeshika simu), Mbunge wa jimbo
la Kilolo Mhe Venance Mwamoto(wa tatu kutoka kushoto), Mbunge wa jimbo
la Kyerwa Mhe Innocent Bilakwate(wa pili kutoka kulia) pamoja na
watumishi wa Halmashauri |
 |
Mkurugenzi Mtendaji Hudson Kamoga akisoma taarifa ya Ukenzi wa Hospital ya Wilaya mbele ya Kamati | |
 |
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Mwita Waitara akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji Hudson Kamoga | |
 |
Naibu
Waziri Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Mary
Mwanjelwa akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji Hudson Kamoga |
Wakati
huo huo Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara ameihakikishia Kamati
hiyo kuwa, Wizara ya TAMISEMI inafuatilia kwa makini ujenzi wa Hospitali
zote 67 za Wilaya zinajengwa kwa awamu ya kwanza kwa ukaribu na
kuhakikisha zinaanza kufanya kazi, pamoja na kuhakikisha ushauri wote
uliotolewa na Kamati unazingatiwa na kufanyiwa kazi.
Naye
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt Chitopela amesema, Hospitali hii ni
tegemea kubwa kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa kuwa
inategemea kuhudumia wakazi zaidi ya 220,000, na kupunguza adha kubwa ya
wananchi wanao safiri umbali mrefu kufuata huduma ya afya. Kwa upande
wa wananchi wa Mbulu wamemshukuru sana Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli
kwa kuwakumbuka na kuwaondolea adha kubwa katika sekta ya afya na hakika
wamepata mkombozi na kiongozi anayejali maisha yao.
No comments:
Post a Comment