Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akisisitiza jambo wakati
akizungumza na Uongozi na watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo
Tanzania (TARI) katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la
Makutupora Jijini Dodoma Leo Tarehe 11 Machi 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt Geoffrey
Mkamilo (Kushoto) akitoa maelezo ya awali kuhusu Taasisi hiyo mbele ya Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya (Katikati) wakati
alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ofisi
za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la Makutupora Jijini Dodoma Leo Tarehe 11 Machi 2020. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti Wizara ya Kilimo Dkt. Wilhelm Mafuru (Kulia)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akisisitiza jambo wakati
akizungumza na Uongozi na watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo
Tanzania (TARI) katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la
Makutupora Jijini Dodoma Leo Tarehe 11 Machi 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt Geoffrey Mkamilo wakati
alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ofisi
za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la Makutupora Jijini Dodoma Leo Tarehe 11 Machi 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akizungungumza na Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la Makutupora Jijini Dodoma Leo Tarehe 11 Machi 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Taasisi
zilizopo Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi za Mazao zimetakiwa kufanya
kazi kwa Bidii na utashi mkubwa ili kutekeleza matakwa na taswira ya
serikali.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya ameyasema hayo Leo Tarehe 11
Machi 2020 wakati akizungumza na Uongozi na watumishi wa Taasisi ya
Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ofisi za makao makuu ya Taasisi
hiyo eneo la Makutupora Jijini Dodoma.
Kusaya
amesisitiza kuwa wataalamu hao wanapaswa kufanya Utafiti na kuonyesha
matokeo chanya ya utafiti huo, Ameongeza kuwa utafiti haupaswi kuishia
kwenye makaratasi pekee bali matokeo chanya kwa wakulima.
Amesema
kuwa Wizara ya Kilimo inashika nafasi ya pili kwa kuwa na wasomi wengi
kwa ngazi za PHD na Maprofesa hivyo taaluma hiyo inapaswa kuwa na
matokeo chanya kwani kutokuwa na matokeo hayo ni kazi bure kwa wananchi
na uwepo wa taasisi hiyo.
Kuhusu
Changamoto ya fedha kwa ajili ya utafiti wa Mazao iliyobainishwa na
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt
Geoffrey Mkamilo, Katibu Mkuu huyo amesema kuwa hakuna mafanikio ya
kilimo bila kuimarisha utafiti hivyo lazima kutafuta njia ya kupata
fedha kwa haraka ili kuendeleza utafiti.
Kusaya
ametoa mwito kwa wafanyakazi wa TARI kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya
kujiendeleza kielimu. "Taasisi ya utafiti ni muhimu sana kwa watu
kujielimisha zaidi, Hata kama una miaka 60 sisi tutakupeleka shule,
hakuna kada ambayo tutaiacha zote tutazipeleka shule ili tuweze kwenda
na wakati" Alikaririwa Katibu Mkuu Ndg Kusaya
Hii
ni ziara ya kwanza ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya
tangu alipokabidhiwa kijiti kuiongoza wizara hiyo kama mtendaji Mkuu
Machi 6, 2020.
No comments:
Post a Comment