Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiongea na Balozi wa Uingereza nchini Mhe.
Balozi Sarah Cooke pamoja na Balozi wa Norway nchini Mhe. Balozi
Elisabeth Jacobsen
Balozi
wa Uingereza nchini Mhe. Balozi Sarah Cooke akimuelezea jambo Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Dkt. Damas Ndumbaro. Katikati ni Balozi wa Norway nchini Mhe. Balozi
Elisabeth Jacobsen.
Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Uingereza nchini Mhe. Balozi Sarah Cooke, Balozi wa Norway nchini Mhe.
Balozi Elisabeth Jacobsen pamoja na Balozi wa Korea nchini Mhe. Balozi
CHO tae-ick.
Dkt.
Ndumbaro amekutana na mabalozi hao leo katika Ofisi ndogo za Wizara
jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili masuala
ya kuongeza ushirikiano wa kidiplomasia pamoja na mikakati ya kujikinga
na kupambana na homa ya virusi vya corona.
Pia,
Mabalozi hao waliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa Kushirikiana na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika
–SADC kwa maamuzi yake ya busara kupitia mawaziri wa Afya ya kuamua
vikao vyote vinavyoendelea kufanyika kwa njia ya mtandao yaani (Video
Conference) ikiwa ni hatua mathubuti ya kukabiliana na maambukizi ya
Ugonjwa huo.
Balozi
wa Norway nchini Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen akimuuliza jambo Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Dkt. Damas Ndumbaro. Kushoto kwake ni Balozi wa Uingereza nchini Mhe.
Balozi Sarah Cooke.
Balozi
wa Korea nchini Mhe. Balozi CHO tae-ick akiongea na Naibu Waziri,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.
Damas Ndumbaro
Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Dkt. Damas Ndumbaro pamoja na Balozi wa Korea nchini Mhe. Balozi CHO
tae-ick wakifuatilia taarifa kuhusu mikakati ya kujikinga na kupambana
na homa ya virusi vya corona
Naibu
Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Dkt. Damas Ndumbaro akimfafanulia jambo Balozi wa Korea nchini Mhe.
Balozi CHO tae-ick
No comments:
Post a Comment