Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Sheikh.Alhajj Burhan Mlau (kulia) na (wa kwanza kushoto ni Sheikh wa Shiha mkoani Arusha, Abubakari Hussein Sombi.
Waziri
Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, juzi ameongoza waislamu katika harambee ya
kuchangia ujenzi wa ofisi ya Baraza la Kuu la Waislamu nchini (BAKWATA)
inayotarajiwa kujengwa eneo la Ilongero, Wilaya ya Singida Vijijini ,
mkoani hapa.
Zaidi
ya shilingi milioni 40 zimepatikana katika vipindi viwili tofauti vya
zoezi la harambee hiyo, ambapo awamu ya kwanza Pinda aliwakilishwa na
Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Sheikh Alhajj Burhan Mlau ambapo
jumla ya shilingi milioni 3.6, sambamba na mifuko 198 ya saruji
vilipatikana.
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu kwenye harambee hiyo.
Awamu
ya pili ya harambee hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki ikiongozwa na
Pinda mwenyewe, ambapo jumla ya shilingi milioni 37 sambamba na mifuko
44 ya saruji vilipatikana na kufanya harambee hiyo kuvuka nusu ya
malengo yake. Jumla ya fedha yote inayohitajika hadi kukamilisha ujenzi
huo ni shilingi milioni 65.5.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani hapa jana, Mlau alimpongeza Waziri Mkuu
mstaafu Pinda na serikali ya mkoa kwa namna wanavyojitoa kikamilifu
katika kusaidia shughuli mbalimbali za dini ya kiislamu kwenye mkoa huo,
na hasa pale muda wote wanapohitajika kufanya hivyo.
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu kwenye harambee hiyo.
“Tunamshukuru sana Pinda kwa kutujali na kututhamini, kwakweli michango yote hii imefanyika kwa hamasa yake na ametuunga mkono kwa nguvu zote,” alisema.
“Tunamshukuru sana Pinda kwa kutujali na kututhamini, kwakweli michango yote hii imefanyika kwa hamasa yake na ametuunga mkono kwa nguvu zote,” alisema.
Aidha,
Mlau alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi ambaye
mara kwa mara hupendelea kumuita “Hajjat” (Mavazi yake siku zote ni
mithili ya mwanamke aliyekwenda hijja) kwa kuwa karibu na dini hiyo ya
Kiislamu na kujitoa kila mara anapohitajika.
Tukio la harambee likiendelea.
Na Godwin Myovela, Singida
“Niwasihi waislamu wenzangu tuwe waaminifu na tutumie michango hii kwa malengo tarajiwa, na pia tunakaribisha wengine wote ambao wangependa kutuunga mkono ili hatimaye tuweze kufanikisha ujenzi huu muhimu,” alisema Alhajj Mlau.
Ujenzi wa ofisi hiyo unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu, baada ya taratibu za maandalizi yake kukamilika.
No comments:
Post a Comment