Waziri
wa wa Mambo ya Nje wa Nepal, Mhe. Pradeep Gyawali alifungua rasmi ofisi
ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Nepal katika hafla
iliyofanyika katika Hoteli ya Radisson Jijini Kathmandu tarehe 02 Machi
2020.
Katika hotuba yake, Waziri Gyawali alieleza kuridhishwa
kwake kutokana na uhusiano thabiti wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi
hizi mbili ambapo zinashirikiana na kujenga hoja zinazofanana kwenye
medani ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande
Wowote, Kundi la 77 na nyinginezo.
Hata hivyo, Waziri Gyawali alielezea umati wa washiriki katika hafla hiyo kuwa kwa sasa, uhusiano huu unapaswa kujikita zaidi katika maeneo ambayo mbia mmojawapo anaweza kunufaika na ujuzi na uzoefu kutoka kwa mwenzake. Akataja maeneo ambayo Nepal imefanikiwa zaidi kama vile utalii wa kupanda milima ambapo Nepal inavyo vilele vya milima nane mirefu kuliko yote duniani ikiongozwa na Mlima Everest.
Awali akimkaribisha Mheshimiwa Waziri Gyawali, Balozi Baraka Luvanda anayeiwakilisha Tanzania nchini India na Nepal alielezea juu ya umuhimu wa ofisi ya Mwakilishi wa Heshima kuwa itasaidia kutoa huduma za Kikonseli kwa karibu zaidi na pia itasaidia kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.
Balozi Luvanda
alitaja maeneo ambayo yanaweza kutazamwa kama ya kuanzia kama vile (i)
Kuwa na Makubaliano ya Mashauriano ya Kisiasa (Political Consultations)
(ii) Kuwa na Makubaliano katika Sekta ya Usafiri wa Anga (Bilateral Air
Services) ambapo “Air Tanzania” inaweza kuingia ubia na “Nepal Airline”
(iii) Kuwa na Makubaliano kwenye sekta ambazo Nepal inafanya vizuri kama
vile Utalii wa kupanda milima na Kilimo.
Bwana Rajesh Chaudhary, raia wa Nepal amekwishaanza rasmi kazi ya Uwakilishi wa Heshima baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kidiplomasia.
Bwana Rajesh Chaudhary, raia wa Nepal amekwishaanza rasmi kazi ya Uwakilishi wa Heshima baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kidiplomasia.
No comments:
Post a Comment