Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Christopher Kadio (kulia), na Mkurugenzi wa Sera na
Mipango, Wanja Mtawazo, wakipanga nyaraka kwa ajili ya kuziwasilisha
katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa,
Bungeni jijini Dodoma, leo. Wizara iliwasilisha katika kikao hicho
Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/21. Picha zote
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Kikao
cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,
kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa, Bungeni jijini
Dodoma, leo. Wizara iliwasilisha katika kikao hicho Taarifa ya
Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/21. Katikati ni Kaimu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Salim Mwinyi Rehani, na kulia ni Katibu wa
Kamati hiyo, Ramadhani Abdalla. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akisalimiana
na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, Hasna Mwilima, nje ya Ukumbi wa
Bunge, jijini Dodoma, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akijipaka
kitakasa mikono (Sanitizer) nje ya Ukumbi wa Bunge, jijini Dodoma, leo,
kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Pius
Msekwa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment