Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Ramadhani Kailima akitumia kitakasa mikono ili kujikijnga na maaumbukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona akiwa katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma |
Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii
Tumeshaambiwa
hakuna sababu ya kutishana kuhusu ugonjwa wa Corona lakini tunahimizwa
kuchukua tahadhari kwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kunawa
mikono mara kwa mara.
Asante
Rais Dk.John Magufuli kwa maelekezo na maagizo yako kwetu Watanzania
katika kipindi hiki ambacho dunia inalia kuhusu Corona.Ugonjwa ambao
ulianzia nchini China na kisha kusambaa nchi mbalimbali duniani.
Kwa
Tanzania kama zilivyo nchini nyingine duniani nayo imekumbwa na
Corona.Cha kumshukuru Mwenyezi Mungu hadi sasa mbali ya kuwa na wagonjwa
wa Corona hakuna aliyepoteza maisha kwa ugonjwa huo.Mungu yuko pamoja
nasi ni matumaini yangu tutavuka salama.
Kabla
ya kuendelea kusoma andiko langu naomba ufahamu kuwa huu ni wakati wa
kila mmoja wetu kwa nafasi yake kuhakikisha anajilinda na
Corona.Kujilinda ni muhimu kwa sasa na hiyo ndio njia rahisi zaidi ya
kujiuepusha nao.
Hata
hivyo lazima nikiri macho yetu yameona mengi tangu kuanza kwa ugonjwa
huu .Masikio yetu nayo yamesikia mengi kuhusu ugonjwa wa Corona. Jambo
la faraja Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake ujumbe umefika.Wanaelewa
kuna Corona.
Ni
jambo jema unapokuwa kwenye jamii na ikatangazwa hatari ukafahamu.Hiyo
peke yake ni hatua namba moja ,ukishajua ni rahisi kuchukua hatua
usidhurike dhidi ya adui.Tanzania Corona iko na sote tunajua.Tuchukue
hatua ya kuudhibiti kwa kuchukua tahadhari.Tujilinde na Corona lakini
msingi ubaki ule ule tusitishane.
Tangu
kuanza kwa Corona kumekuwa na mijadala mingi mtaani kwetu.Nadhani hata
huko kwako nako mijadala inaendelea.Iko ile inayohusisha watalaam wa
afya kwa maana ya kutoa maelekezo na miongozo.Pia iko mijadala
inayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto.Lengo ni kuhakikisha tunakuwa na uelewa.
Pia, kuna mijadala inayohusisha akina sie pangu pakavu tia mchuzi.Hatuna tunachokijua lakini tumekuwa wazungumzaji hodari.
Nikiri
kuna mijadala ambayo inazungumzia Corona na hii kwa sehemu kubwa imejaa
mzaha na utani wa kila aina.Kwenye mijadala ya mzaha na utani ,
Serikali inatakiwa kuchukua hatua.
Ni
hatua za aina gani yenyewe inajua, sina nafasi ya kutoa maelekezo kwa
Serikali yangu bali nina kila sababu ya mimi na wengine kupokea
maelekezo.
Hata
hivyo katika kusikia yanayozungumzwa hivi sasa, namshukuru Mungu
nimepata nafasi ya kumsikia Rais Dk.John Magufuli na hasa hotuba yake
kuhusu Corona.Ni hotuba ambayo imejaa kila aina ya maelekezo na maagizo
na kubwa zaidi inaonesha matumaini kwa Watanzania wote.Rais ametoa
maelekezo ya kukabiliana na Corona.
Kubwa
ambalo amenikosha , pamoja na kuchukua tahadhari amesisitiza umuhimu wa
Watanzania kuendelea kuchapa kazi.Hili la kufanya kazi ni jambo la
msingi kwani pamoja na kuwa na tatizo la Corona, lakini maisha lazima
yaendelee.
Nimesikia
baadhi ya watu wakitaka Watanzania nao wazuiliwe kutoka nje kama sehemu
ya kujikinga na Corona.Ukiulizwa kwani wanakwambia mbona nchi nyingine
wamechukua hatua za aina hiyo.
Sawa
nchi nyingine zimeamua kuzuia watu wake wasitoke nje.Lazima tukubali
kila nchi inautaratibu wake wa kukabiliana na Corona.Hatuna sababu ya
kuiga nchi nyingine imefanya nini na badala yake tunatakiwa kuchukua
hatua kulingana na mazingira ya watu wetu.
Unaweza
kuchukua hatua kama ambazo wamechukua China mwisho wa siku nchi
ikaingia kwenye janga kubwa zaidi. Isitoshe Corona ni ugonjwa ambao
umegundulika mwaka 2019 na ndio maana unafahamika kwa jina la COVID-19
(Corona).
Ni
wajibu wetu kama Taifa kujipanga na kuchukua hatua kulingana na
maelekezo ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na
Watoto.Tukifanya hivyo tutavuka salama.Haitakuwa na maana tuko Tanzania
halafu tunataka kukabiliana na Corona kwa kuchukua hatua ambazo Marekani
imechukua.Wananchi wa Marekani wanafuata ambacho kimesemwa na Rais wao
na Serikali yao.Nasi tunatakiwa kuchukua maelekezo ya maagizo ya Rais
wetu na Serikali yetu.
Naomba
nisisitize Rais Magufuli binafsi nimekuelewa na naamini Watanzania
wamekuelewa.Tutachukua tahadhari kwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya
lazima, tutajiepusha na mikutano, warsha na makongamano hadi pale
tutakapopata maelekezo mengine ya Serikali.
Shule
zimefungwa , sote tunafahamu.Ukweli tutaendelea kufanya kazi kwa
bidii.Nikiri tangu kuanza kwa Corona kuna mambo mengi yamesimama kwa
baadhi ya shughuli.
Ni
changamoto lakini ni jukumu letu kupambana na changamoto zote
zinazojitokeza sasa.Mungu Muumba wa Mbingu na Ardhi hakika siku zote
amekuwa pamoja nasi.Rais wangu nimekusikia ukisisitiza umuhimu wa
kufanya ibada katika kipindi hiki tumekusikia na tutaendelea kufanya
ibada.Ni jukumu la kila mwanadamu kuhakikisha anakuwa karibu na Mungu
maana sote tumaini letu ni kwake.Tanzania nchi yangu.Tanzania
nakupenda.Mungu tuepushe Watanzania dhidi ya Corona.
No comments:
Post a Comment