Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi (katikati, na wajumbe wa Jukwaa la Haki Jinai mkoa wa Singida, muda mfupi baada ya mkuu wa mkoa kulizindua rasmi.
Idadi
ya waliofutiwa Mashtaka na Ofisi ya Mashtaka ya Taifa kwa makosa
mbalimbali kwenye magereza ya wilaya za Manyoni na Iramba mkoani hapa
sasa imefikia 99.
Watuhumiwa
85 walioachiwa kwenye gereza la Manyoni ni wale wenye makosa
yanayohusiana na kesi za uhujumu uchumi, udanganyifu na rushwa, huku 14
wa gereza la Iramba Kiomboi ni wale wa makosa mchanganyiko.
Akiwa
kwenye ziara ya kutembelea wadau wa ‘Haki Jinai’, mkoani hapa, hivi
karibuni, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, alisema
baada ya kutembelea magereza husika, kuangalia mwenendo mzima wa
upelelezi na wapelelezaji, na kupata fursa ya kusikiliza mahabusu
mbalimbali na kujiridhisha ndipo alipoamua kufuta kesi hizo.
“Nimefuta
kwa wale ambao nimejiridhisha kwamba kesi zao hazina sababu ya kukaa
gerezani, na hawa wengine wa uhujumi uchumi ni ambao waliingia kwenye
hifadhi ya Rungwa wakiwa na mitambo na kuchimba madini, baada ya kukiri
mbele yangu kwamba ni kweli wamefanya hayo makosa na ukiangalia gereza
limejaa nikaona na wenyewe niwapatie nafasi ya mwisho,” alisema Mganga.
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Biswalo Mganga (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi na Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Angelina Lutambi muda mfupi baada ya hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Haki Jinai ngazi ya Mkoa.
Na Godwin Myovela, Singida
Alisema, lengo hasa la ziara yake kwa wadau ilikuwa ni kufanya ukaguzi wa kesi zinazohusiana na rushwa na udanganyifu, kukagua kama kesi hizo zinaendeshwa na kupepelezwa ipasavyo, na kama kuna tija na matokeo tarajiwa, lakini pia kama kuna changamoto.
No comments:
Post a Comment