Shilingi
Bilioni 18.62 zilivyowezesha mageuzi ya
miundombinu ya barabara za lami katika Manispaa ya Kigoma Ujiji .
Akizungumzia
utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi wa Manispaa hiyo Injinia Wilfred Shimba amesema kuwa barabara zilizojengwa zina urefu
wa Kilomita 12 na ujenzi huo umehusisha
njia za waenda kwa miguu, mifereji ya maji na taa za barabarani.
“
Awali Manispaa ya Kigoma Ujiji ilikuwa na barabara moja tu yenye lami na kwa
sasa kujengwa kwa barabara hizi kunachangia kukuza shughuli za kiuchumi na
hivyo hata mapato yanaongezeka na mandhari ya mji inavutia zaidi kwa sasa”,
Alisisitiza Mhandisi Shimba
Barabara zilizojengwa
kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kama inavyoonekana katika
picha.
|
Akifafanua
Mhandisi Shimba amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za Manispaa hiyo
umekuwa chachu ya maendeleo katika Manispaa hiyo na imevutia na kuchangia kuongezeka kwa shughuli za
kiuchumi kwa wananchi.
Alizitaja
faida za mradi huo kuwa ni pamoja na; kurahisisha usafiri na usafirishaji ndani
ya Manispaa hiyo, kuvutia uwekezaji, kufanya Manispaa hiyo kuwa na muonekano
bora zaidi ya ilivyokuwa awali kabla ya kuboreshwa kwa miundombinu hiyo ikiwemo
kuwekwa kwa taa za kuongozea magari.
Akizungumzia
utekelezaji wa mradi huo umekamilika na kuanza kuleta manufaa kwa wakazi wa
Kigoma na wawekezaji wote wanaofika katika Manispaa hiyo kwa lengo la kufanya
uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuchangia katika kukuza uchumi na ustawi
wa wananchi.
Muonekano wa moja ya
barabara za Manispaa ya Kigoma Ujiji baada ya kujengwa kwa kiwango cha lami
kama ilivyokutwa nyakati za usiku Machi
29, 2020.
(Picha
zote na Aboubakari Kafumba MAELEZO-
Kigoma)
|
Na Frank
Mvungi- MAELEZO Kigoma
Kwa
sasa baada ya kukamilika kwa kazi zote ambazo zipo katika mkataba wa ujenzi wa
barabara ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua, imeleta tija
katika sehemu zote za maeneo ya mradi, hususani mfereji wa maji yam vu wa
Katonyanga na barabara zote ili kupunguza adha za maji ya mvua kwa wakazi wa
maeneo yote ya Manispaa ya Kigoma.
Kwa
upande wake mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji
Bw. Yasin Ally amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mageuzi
kwa makubwa katika ujenzi wa miundombinu ya Manispaa hiyo zikiwemo barabara za
lami, taa na huduma za jamii zimeimarishwa.
Aliongeza
kuwa kuimarishwa kwa miundombinu ni
chachu ya maendeleo kwa wananchi wa mkoa huo kwa ujumla.
Ujenzi
wa barabara za lami katika Manispaa ya Kigoma Ujiji umefanyika katika mitaa ya
Kaaya hadi Simu, Mwanga Kitabwe
Mwembetogwa, Wafipa Kagera, Kagashe Road, Kukolwa Road, Ujenzi Nazareth, Maweni Burega.
No comments:
Post a Comment