Matokeo chanyA+ online




Wednesday, April 15, 2020

RIDHIWANI AIKABIDHI HALMASHAURI YA CHALINZE MABATI, MATANKI YA MAJI YENYE GHARAMA YA MIL.13.9

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

Mbunge wa Jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amekabidhi mabati 1,000 kwa halmashauri ya Chalinze ,pamoja na tanki za maji na mabeseni Tisa vyote vikiwa na gharama ya milioni 13.9.

Kati ya mabati hayo 600  yataelekezwa katika miradi ya halmashauri ya sekta ya elimu na afya na 400 yatapangiwa kazi na matakwa ya mfuko wa jimbo. 

Akizungumzia kuhusu msaada huo ,Ridhiwani alieleza kuwa , shule ya sekondari Changarikwa inapatiwa mabati 90,Msata 90,Chamakweza mabati 90,nyumba ya mwalimu sekondari ya Lugoba mabati 30 na shule ya msingi Magome mabati 60, Msolwa 60,Kidogozero mabati 90 na Ruvu Darajani.

Alisema,matanki ya maji yanakwenda katika vituo vya afya,zahanati ili kujikinga na janga la ugonjwa wa corona.

Ridhiwani alieleza ,kwasasa jamii inapaswa kujihadhali na ugonjwa huo hivyo akaona umuhimu wa kutafuta mdau Shubash Patel ambae alitoa matanki tisa aina ya Kiboko pamoja na mabati kwa ajili ya kuezeka miradi ya afya na elimu jimboni hapo .

"Kuna maeneo ya mkusanyiko mahitaji bado ni makubwa ya ndoo za maji kwaajili ya wananchi kunawa maji ,kama pale mnada wa Bwilingu ,nilitembelea wiki iliyopita mahitaji ni makubwa " alisema Ridhiwani.

Kutokana na hilo pia amempata mdau mwingine ambae atamsaidia kuleta ndoo 30 kwa ajili ya kulinda na corona pamoja na makopo ya rangi na gymsum:;anasema Ridhiwani.

No comments:

Post a Comment